Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI YA USIKU HUU: HI NDIO TAARIFA RASMI KUHUSU HALI YA GWJIMA BAADA YA KUKAA KUSIKOJULIKANA HATIMAE SASA UKWELI WA MAMBO HUU HAPA....

Askofu Mkuu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima
PETER Kibatala wakili wa Josephati Gwajima Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima ameiomba mahakama kuhairisha tarehe ya kusikiliza kesi inayomkabili askofu huyo sababu anaumwa,anaandika Faki Sosi.
Kibatala amedai mahakamani Kisutu kuwa kutotokea kwa mteja wake leo kumetokana na yeye kuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Wakili huyo mtaratibu mwenye hoja aliwasilisha madai hayo leo katika Mahakaama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Syprian Mkeha Hakimu Mfawidhi anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili Gwajima
Mahakama imekubali ombi hilo na kwamba kesi hiyo itatajwa tena 2 Agosti mwaka huu.
Katika kesi hiyo Gwajima anadaiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam.
Gwajima anadaiwa kufanya tukio hilo kati ya 16 na 25Machi, mwaka 2015 katika Viwanja vya Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top