Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

Ronaldo Aifikia Rekodi ya Mfunguaji wa Mabao wa Muda Wote wa Michuano ya EURO


Cristiano Ronaldo inawezekana hafanyi vizuri kwenye michuano ya Euro 2016, lakini licha ya kutocheza katika kiwango chake kinachotarajiwa, bado anauwezo wa kutengeneza na kuvunja rekodi.

Kuvunja rekodi imekuwa ni sehemu ya maisha ya ronado, mara kadhaa amefanya hivyo kwenye klabu yake ya Real Madrid, baada ya goli lake la kichwa dhidi ya Wales amefanikiwa pia kufikia rekodi iliyowekwa na Michel Platini miaka kibao iliyopita.

Ronaldo aliruka juu mithili ya mcheza kikapu Lebron James na kukutana na krosi ya Gueirrero kisha kuuzamisha mpira kambani.Goli hilo liliipa Ureno uongozi wa goli 1-0 dhidi ya Wales kwenye mchezo wa nusu fainali ya Euro 2016 na kumfanya Ronaldo awe sambamba na rekodi ya legend wa Ufaransa Michel Platini ya kufunga magoli magoli 9 kwenye michuano ya Mataifa ya Ulaya.

Ronaldo alifunga goli lake la kwanza kwenye michuano ya Euro mwaka 2004.

Anahitaji goli moja ili kuwa mfungaji wa muda wote kwenye michuano ya Euro.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top