Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

Video: Aunt Lulu Afanya Ufuska Kweupe!

auntlulu1
Staa wa Filamu za Kibongo na mtangazaji, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’.
Kujitoa ufahamu! Ndivyo alivyofanya Mtangazaji Lulu Semangongo ‘Aunt Lulu’ baada ya kukutwa akifanya vitendo vya kifuska hadharani bila tone la aibu.
Mtangazaji huyo alikutwa akifanya uchafu kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar alipokuwa amejumuika na mastaa wa Kundi la Scorpion Girls, Isabela Mpanda, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuzi’ ambapo alikuwa akinywa vinywaji vikali na kuvuta sigara. Timu yetu ya Operesheni Fichuo Maovu (OFM) ilimshuhudia Aunt Lulu akiwa amelewa bwii huku akimkatia mauno mwanaume mmoja bila kujali wingi wa watu waliokuwa eneo hilo.

 Aunt Lulu akiwa katika pozi.
OFM walimrekodi video Aunt Lulu ambaye muda wote alikuwa akizungumza maneno yalioshiria kuzidiwa na kilevi kichwani. Ukiacha ulevi wa sigara na pombe, mwanadada huyo alitia fora baada ya kumgeukia mwanaume huyo aliyekuwa naye kisha kufanya naye mambo ya chumbani hadharani hivyo kusababisha wenye aibu zao kutazama pembeni.
Baada ya kufanikiwa kumrekodi video na kushindwa kuzungumza naye kutokana na hali hiyo ya ulevi, siku iliyofuata mwandishi wetu alimtafuta Aunt Lulu ili kumuhoji sababu ya kujiachia na kutouthamini mwili wake kwa kuvuta sigara na kunywa pombe kali lakini hakupokea simu siku nzima. Gazeti hili linaendelea kumtafuta atakapopatikana atabanwa ili kujua kama kuna kitu kinamsibu hadi aamue kunywa pombe na kuvuta sigara kiasi cha kufanya vitendo vya aibu hadharani.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top