Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

BREAKING NEWS: HAKUNA ALIEAMINI HAYA RAIS MAGUFULI AMGARAGAZA VIKALI MH LOWASSA..

lowassa
Mwaka mmoja baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu nchini, utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonesha kuwa Rais John Magufuli amewazidi umaarufu kwa mbali wanasiasa waliogombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kampuni ya Mwananchi Communication kwa kutumia Infrotrack, Dkt. Magufuli alipata asilimia 54.6 akifuatiwa na Edward Lowassa (Chadema) ambaye aliyepata asilimia 27 akifuatiwa na Anna Mghwira (ACT – Wazalendo) aliyepata asilimia 2.3 huku wengine wakipata chini ya asilimia 1.
“Watu 1,000 walihojiwa kama sampuli ya watu wazima zaidi ya 24,253,555 wenye umri zaidi ya miaka 18 kutoka katika kata 113 zilizoko katika mikoa 15 ya kanda zote sita,” Mwananchi wameeleza.
Magufuli amevunja rekodi ya Lowassa ambaye kabla ya kuanza mchakato wa kutafuta wagombea wa nafasi za urais, akiwa bado yuko CCM aliongoza kwa mbali katika utafiti wa watu maarufu na wenye nguvu zaidi kisiasa wanaopewa nafasi ya kushinda uchaguzi huo. Katika utafiti huo, jina la Dkt. Magufuli halikuwa sehemu ya waliopewa nafasi.
Dkt. Magufuli alishinda urais kwa kupata kura zaidi ya milioni 8 akifuatiwa na Lowassa aliyepata zaidi ya kura milioni 6, katika uchaguzi ambao uliweka historia ya ushindani mkali ambao haukuwahi kushuhudiwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.
Hata hivyo, watafiti wa Infrotrack wamesema, “mchuano kati ya Magufuli na Lowassa bado ni mkali.”

1 comments:

aachwe afanye siasa tuone mbona akishuka tuu kwenye basi polisi wanamshika eti mchochezi

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top