Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

BREAKING NEWS: PIGO ZITO KLABU YA SIMBA YAFIKIA MAAMUZI MAZITO MSIMBAZI HAKUKALIKI..


Joseph Omog ametangaza kuifumua ngome ya timu hiyo pamoja na kipa akilalamikia aina ya mabao wanayofungwa baada ya timu yake kuchapwa mabao 2-1 na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Huo ni mchezo wa pili mfululizo kwa Simba kupoteza, ilichapwa bao 1-0 na African Lyon, wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru.
“Nitakwenda mapumziko, lakini mabeki na kipa wameniangusha sana, nitaanza nao ...nitaifumua ngome, huwezi kufungwa mabao kwa staili moja, sisi tumefungwa mabao matatu kwa staili moja na bao la African Lyon,” alisema Omog aliyekuwa akionekana haamini kilichotokea.
Alisema mabeki wanashindwa kujipanga wakati kipa anabaki golini badala ya kutoka kucheza mipira inayokuja golini na anafungwa mabao mepesi.
Mchezo ulivyokuwa


Kipigo hicho cha Simba kimetoa mwanya kwa Yanga kuwakaribia kileleni leo itakapocheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru.
Simba inaizidi Yanga pointi tano kabla ya mechi ya mabingwa watetezi na endapo itawafunga Ruvu basi watakuwa wanabakiza pointi mbili kuwafikia kileleni.
Simba ilitangulia kuliona lango la Prisons dakika 41 lililofungwa na Jamal Mnyate aliyepokea krosi ya Shiza Kichuya na kuuzamisha mpira nyavuni kwa kichwa.
Dakika ya 48 Victor Hangaya aliisawazishia Prisons bao kwa kichwa baada ya kupokea krosi ya Salum Kimenya na kufanya mchezo wa ushindani.
Hangaya aliipatia Prisons bao la pili dakika 68 na kuwaweka wachezaji wa Simba, kucheza kwa presha kubwa hadi kupoteza mchezo huo.
Mabadiliko ya Simba dakika ya 68 kumtoa Kazimoto na kumuingiza Mohamed Ibrahim yalisaidia kuongeza nguvu ya mashambulizi ingawa hayakuweza kufikia lengo la kupata bao.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top