Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI NZITO USIKU HUU: DUNIA YASHTUKA PAPA FRANSISCO AISHTUA DUNIA KWA KAULI YAKE HII...

Image result for papa francisco

Jamii imeaswa kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu, weledi na uzalendo wa hali ya juu ili wapate kuheshimika na kuthaminiwa na jamii zinazowazunguka kwa kutambua mchango wao katika kuendeleza jamii.

Hayo yamesemwa na Mhadhama Kardinali Polycup Pengo wakati wa hafla ya kumkabidhi nishani ya Benemerenti (Anayestahili), Dk. Fredrick Kigadye, ambayo hutolewa na Baba Mtakatifu kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kulitumikia Kanisa na jamii kwa ujumla, Jijini Dar es Salaam.

“Ni vyema tukatambua ya kwamba kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ndiyo msingi mkuu wa mafanikio mahali pepote pa kazi na katika maisha yetu ya kila siku”. Alisema Kardinali Pengo.

Kwa upande wake Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa amesema kuwa Dk. Kigadye amekuwa mtumishi wa wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa muda wa miaka 35 huku akifanya kazi katika Idara ya Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa mafanikio makubwa.

Ameonesha ni namna gani watu tunapaswa kujitoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu kupitia vipawa na taaluma tulizo jaaliwakuwa nazo hii inatia moyo sana. Aliongeza Askofu Ngalalekumtwa.

Akizungumzia Tuzo hiyo aliyopewa na Baba Mtakatifu Papa Francis, Dk. Kagadye amesema kuwa anajisikia mwenye furaha kubwa na wathamani kwa kupewa tuzo ya heshima na kiongozi mkubwa duniani nakuongeza kuwa tuzo hiyo inamuongezea chachu ya kuishi katika misingi imara ya maadili na weledi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top