Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI NZITO USIKU HUU: KIVUMBI KIMEWAKA USIKU HUU SERIKALI YAFIKIA MAAMUZI MAZITO JUU YA KAMPENI HII NYETI KUWAHI KUTOKEA NCHINI..

Katika kuhakikisha uwajibikaji wa watumishi wa Umma unaimarika kwa kuzingatia Maadili, haki za binadamu na utawala bora Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi  wa Umma na utawala bora  amezindua kampeni ya mwezi mmoja yenye lengo la kusimamia maadili na uwajibikaji zaidi.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo Waziri wa Nchi ofisi ya Rais, Utumishi  wa Umma na utawala bora  Angella Kairuki amesema kuwa lengo kuu la Kampeni hiyo ni kuhakikisha kuwa taasisi zote za umma na binafsi nchini zinazingatia na kujenga maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa ili kujenga usawa miongoni mwa wanajamii katika kuelekea Siku ya Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za binadamu tarehe 10 mwezi Disemba.

Aidha Kairuki ameongeza kuwa Dhumuni la maadhimisho hayo ni kuliwezesha Taifa kusimamia na kutekeleza kwa vitendo dhana na misingi ya maadili, Haki za binadamu, utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa.

Naye Mkurugenzi mkuu wa Takukuru Valentino Mlowola amesema watatumia kampeni hiyo kuelimisha jamii juu ya madhara ya rushwa ambayo imekuwa tatizo sugu ulimwenguni huku likigharimu zaidi maisha ya wanyonge.

Katika kampeni hiyo imeunganisha taasisi kadhaa ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Rais Menejment ya Utumishi wa Umma na  Utawala Bora (Idara ya Ukuzaji wa Maadili), Ofisi ya Rais- Tume ya Utumishi wa Umma (PSC), Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG), Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (ES).

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top