Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI YA KUSIKITISHA: HILI NI PIGO KALI KWA CHADEMA NA TANZANIA YOTE MASIKINI MH LEMMA YAMKUTA MAZITO JIONI HII..

lema
Kwa mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi miwili, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amefunga ili kuwa karibu na Mungu wakati akiendelea kushikiliwa na polisi mkoani Arusha.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo na hata alipotafutwa kwa simu, hakupokea.
Suala la Lema kuacha kula ili awe  karibu zaidi na Mungu limeelezwa na mwenyekiti wa Chadema wa mkoa, Amani Golugwa ambaye amesema ameelezwa na mke wa mbunge huyo.
Lema, ambaye alikamatwa Jumatano iliyopita mkoani Dodoma na kuletwa mjini hapa Alhamisi, bado hajafikishwa mahakamani.
Imeelezwa kuwa viongozi wa chama chake wameshindwa kumuona kutokana na kuzuiwa na polisi.
Golugwa amesema amepokea ujumbe kutoka kwa mke wa mbunge huyo, Neema Lema kuwa mumewe ameamua kufunga na kuomba kwa ajili ya Taifa kuhusu mambo yanayoendelea na kuwa ameona kipindi hiki ambacho yupo rumande ni cha kuwa karibu zaidi na Mungu.
“Kama tunavyomjua Lema ni mtu anayempenda sana Mungu, ameamua kujinyenyekeza mbele za Mungu. Anafunga na kuomba jioni mke wake anampelekea chakula na amesema yupo katika hali nzuri,” amesema Golugwa.
Amesema wamejitahidi kutaka kumuona Lema, lakini wamegonga mwamba na wameshindwa kumwekea dhamana mbunge huyo.
“Ni jambo la kushangaza kama mtuhumiwa anaweza kukaa rumande zaidi ya saa 48 kama sheria inavyotaka, nadhani hapa siyo sheria tena, labda ni kwa mujibu wa maelekezo ambayo hatujui yametoka wapi na kwa malengo yapi,” amehoji Golugwa.
Juzi, Kamanda Mkumbo alisema Lema hataachiwa hadi upelelezi ukamilike na mwanasheria wa Serikali atakapokuwa amemaliza kuandaa mashtaka kwa kuwa amekuwa akirudia makosa yaleyale ya uchochezi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top