Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI YA KUSIKTISHA USIKU HUU: MWALIMU AFUMANIWA AKIMBAKA MWANAFUNZI WAKE SHUHUDIA TUKIO HILI HAPA...


Taarifa zaidi zilidai kuwa wanafunzi walioshiriki fumanizi hilo dhidi ya mwalimu na mwanfunzi mwenzao walimuadhibu mtuhumiwa (mwalimu) wao na kufanikisha kukamatwa kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, aliiambia Nipashe jana kuwa atalitolea ufafanuzi suala hilo baada ya kupokea taarifa rasmi.
Hata hivyo, inaelezwa na mashuhuda kuwa mwalimu huyo alitiwa mbaroni usiku wa kuamkia jana na wananchi pamoja na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Songa wilayani humo, Juma Bendera, ambaye alipata taarifa kwamba mwalimu amemfungia mwanafunzi chumbani mwake.
Akizungumza na Nipashe jana, Afisa Mtendaji huyo alisema juzi saa tano usiku, alipata taarifa kuwa katika shule hiyo ya Songa kuna mwalimu aliyemfungia mwanafunzi wake wa kike chumbani.
Alisema baada ya kupata taarifa hiyo, alifika shuleni ambapo alimkuta mkuu wa shule hiyo, Habibu Shedafa na mwenyekiti wa Wazazi wa shule hiyo, Rashidi Madiwa, na kundi la wanafunzi wavulana wakiwa eneo la nyumba ya mwalimu huyo huku mtuhumiwa akiwa ndani na mwanafunzi huyo wa kike.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wazazi wa shule hiyo, Rashidi Madiwa, alisema baada ya kupata taarifa hizo, alikwenda katika nyumba anayoishi mwalimu huyo na kupitia dirishani aliwaona yeye (mwalimu) na mwanafunzi wakiwa watupu kama walivyozaliwa huku wakinyonyana ndimi zao.
“Milango ya nyumba ilifungwa, tulipochungulia dirishani tulimuona mwalimu na mwanafunzi wamevua nguo zote na wananyonyana ulimi… ni jambo linaloshitua na kuumiza hasa kwa kuzingatia mwalimu ni mtu muhimu katika jamii,” alisema Madiwa.
Alisema walipojaribu kumuita ili atoke nje, alikataa na ndipo kundi la wanafunzi wavulana wakaamua kuvunja mlango wa nyumba na kufanikiwa kuingia ndani.
Alisema wanafunzi walishindwa kumkamata mwalimu huyo baada ya kuwatishia kwa panga na hatimaye kupata nafasi ya kukimbia hadi katika nyumba ya mwalimu mwenzake.
Alisema hatua yake hiyo haikumsaidia kufuatia wanafunzi kumfuata huko na kuangushia kipigo kabla ya kumuweka chini ya ulinzi na kisha polisi kuja na kumchukua.
CHANZO KUNASWA
Ilielezwa kuwa kabla ya mwanafunzi huyo kwenda kwenye nyumba ya mwalimu, alikuwa akitumiana ujumbe mfupi wa simu ya mkononi na mwalimu wake huyo.
“Katika ujumbe huo, mwalimu alimwambia mwanafunzi atoroke nje ya bweni lao na aende nyumbani kwake wakafanye mapenzi, “ alieleza mtendaji Bendera.
Alisema baada ya mwanafunzi huyo kufanikiwa kutoroka alielekea moja kwa moja nyumbani kwa mwalimu huyo na kuingia ndani.
Alisema baadhi ya wanafunzi anaoishi bweni moja baada ya kuhakikisha mlango umefungwa, walianza kutoa taarifa sehemu mbalimbali ikiwamo kwa mwenyekiti wa kitongoji cha ambaye alikuja kuungana nao kumtoa.
Mwanafunzi aliyehusishwa na tukio hilo, amefanyiwa vipimo katika Zahanati ya Songa, na baadae alipelekwa polisi kwa ajili ya mahojiano.
Diwani wa kata ya Songa, Leslie Nchimbi, alilaani kitendo hicho na kusema ni imani yake kuwa hatua kali zitachukuliwa ili kukomesha uvunjifu huo wa maadili ya kazi ya ualimu na pia ya kijamii.
Naye Mkuu wa wilaya ya Muheza, Mwanasha Tumbo, ametoa onyo kwa vijana na walimu wa shule hiyo, kuacha mara moja tabia ya kujihusisha mapenzi na atakayegundulika atakamatwa na kufunguliwa mashtaka. Mkuu wa shule hiyo, Habibu Shedafa, amethibitisha kutokea tukio na kueleza kuwa juhudi zinafanyika kuhakikisha matukio ya aina hiyo yanakomeshwa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top