Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

KUTOKA BUNGENI KIMENUKA TENA BUNGENI KAMBI YA UPINZANI BUNGENI WAFANYA TUKIO ZITO ZIDI MH NAPE..


Mvutano mkali umetokea bungeni baina ya Serikali na Kambi ya Upinzani katika baadhi ya vifungu vya Muswada wa Sheria ya Huduma ya Habari ikiwamo mamlaka aliyopewa waziri.
Muswada huo ambao umekuwa ukipigiwa kelele na wadau wa sekta ya habari nchini, huku wakitaka muda zaidi kwa ajili ya kuuchambua uliwasilishwa jana bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akieleza kuwa Serikali imeufanyia maboresho.
Nape katika uwasilishaji wake, ametaja maboresho ya muswada huo kuwa ni pamoja na kutoa haki ya kupinga mahakamani aliyekataliwa kupewa leseni ya vyombo vya habari.
Amesema katika kifungu cha 10 kuhusu utoaji wa leseni za vyombo vya habari, muswada wa awali haukuwa umeweka haki ya atakayekataliwa kupewa leseni na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) kukata rufaa.
“Kifungu hiki kimeboreshwa sasa umewekwa mfumo wa wazi zaidi na wa kidemokrasia ambapo uamuzi wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) hautakuwa wa mwisho,”amesema.
“Chombo husika kinakata rufaa kwa Waziri wa Habari na kisiporidhika na uamuzi wa waziri sasa kinaweza kupinga suala hilo mahakamani,” amesema.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top