Uzalendo ni kutokubali na kutonyamaza kimya wakati rais wako anaposemwa vibaya kwa hoja za uongo na media za nchi nyingine, bali ni kwa media zetu kujitokeza, kuukanusha uongo kwa kuusema ukweli na ikibidi serikali yetu sio tuu ikanushe bali pua ihitaji kuombwa radhi!.
Pamoja na matatizo yote na mapungufu yote ya rais wetu Magufuli, kwa sababu na yeye ni binadamu na sio malaika, Watanzania wote wazalendo wa kweli wa nchi yetu, tusikubali rais wetu
kudhalilishwa kwa kusemwa vibaya, na kusingiziwa uongo na media za nje bila ya media za ndani kukanusha na kumtetea, au kuunyamazia udhalilishaji kama huu ni sawa na kushangilia rais wetu kudhalilishwa.
Wito.
Any bad publicity kumhusu rais wetu ni bad publicity kuhusu nchi yetu, natoa wito kwa wazalendo wote kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kutokubali au kushabikia bad publicity kuhusu nchi yetu. Think of multiplier effects za bad publicity!. Its not good kwa investment climate, tunapoelekea kwenye Tanzania ya viwanda, its not good for tourism yetu. It's not good for Tanzania in general kwenye international arena, not good at all.
Hivyo natoa wito maalum kwa Waziri wa Habari, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu au Idara ya Habari Maelezo kuukanusha uongo huu unaoenezwa kumhusu rais wetu, kwa sababu uongo ukisemwa sana na kuachwa bila kukanushwa mwishowe sio utaonekana kama ni ukweli, bali utageuka ukweli.
Jumatatu Njema.
Post a Comment