Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI NZITO: MAZITO YAIBUKA HAKUNA ALIETEGEMEA MKE WA ROMA NA SIRI NZITO MNO YA KUTEKWA KWA ROMA

ya madai ya mumewe ambaye ni staa wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ kutekwa na kuteswa kisha kutelekezwa akiwa na wenzake watatu baada ya siku kadhaa, mke wa jamaa huyo aitwaye Nancy ameacha gumzo kufuatia ujasiri aliouonesha katika tukio hilo.
Kwa mujibu wa watu wa karibu na familia ya Roma, Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyezaa na Roma aitwaye Ivan, alionesha ujasiri wa aina yake kwani alikuwa halali badala yake alizunguka kila kona jijini Dar akimsaka mumewe, jambo ambalo baadhi ya wanawake wasingeweza kulifanya.
“Nancy siyo wa mchezomchezo, tangu mumewe alipotekwa alikuwa halali. Alichokifanya aliomba msaada kwa ndugu zake wa kumtafuta mumewe kila kona hadi alipopatikana.
“Unaambiwa alizunguka kila sehemu bila mafanikio akimtafuta mume wake tangu aliposikia taarifa za kutekwa usiku wa Jumatano (wiki iliyopita). “Nancy alianzia Studio za Tongwe Records (Masaki), baada ya hapo hakulala, alizunguka karibia vituo vyote vya polisi Dar.
Alituma watu hadi mochwari kumuulizia mumewe na wakati huohuo akiviomba vyombo vya habari kumsaidia hadi mumewe alipopatikana, tofauti na wanawake wengine ambao wangejifungia tu kusubiri taarifa.
“Unajua watu wengi walikuwa hawamjui Nancy ni mtu wa aina gani lakini tukio la Roma limemfanya awe gumzo sana kwa ujasiri aliounesha kwenye kipindi kigumu alichopitia,” alisema mtu huyo wa karibu wa familia ya Roma. Akizungumza na Amani juu ya ujasiri aliouonesha kwenye tukio hilo, Nancy alisema kuwa, tukio hilo lilimfanya achanganyikiwe na kujikuta akihangaika kwenye vituo vingi vya polisi jijini Dar. Alisema kuwa, kilichokuwa kinamfanya achanganyikiwe na kushindwa kupata usingizi ni kwamba, kabla, hakuwahi kumpatia taarifa yoyote kama anatafutwa na polisi achilia mbali kuwa na tatizo na mtu yeyote.
Hata hivyo, Nancy aliwashukuru wadau mbalimbali pamoja na Watanzania kwa ujumla kumuunga mkono katika jitihada za kumtafuta mume wake hadi alipopatikana na bado wameendelea kutoa pole hivyo kuonesha upendo mkubwa walionao kwa baba mtoto wake.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top