Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI NZITO YA HIVI PUNDE MH ZITTO KABWE ACHANGANYIKIWA NA UNGA WABUNGE WENZIE WAFUNGA MAZITO MNO.

Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema bei ya unga wa ugali sasa ni juu kuliko hata bei ya mafuta ya magari jambo ambalo linafanya wananchi kuumia na gharama hizi za chakula.

Zitto Kabwe amesema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook na kusema bei hizi za chukula zipo juu sana na kufanya wananchi kuingia kwenye umasikini  

"Bei ya Unga wa Sembe 1kg TZS 2,300/= ( wastani ). Bei ya Mafuta ya Petroli 1lita TZS 2,060/= ( wastani). Kwa mara ya kwanza Ugali umekuwa ghali kuliko mafuta ya gari. Gharama hizi za maisha Kwa wananchi ni kubwa mno, hazistahmiliki na zinaingiza raia wengi kwenye umasikini. Serikali ipo kimya kana kwamba kila kitu kipo sawa" alisema Zitto Kabwe 

1 comments:

Kilicho cha ajabu nini?. Nadhani afadhari unga uwe bei juu kuliko mafuta. Mara zote waliokuwa maskini ni wakulima kwa sababu ya bei ndogo ya mazao yao hivyo kama bei ya unga ni kubwa ina maana wakulima wetu watafaidi zaidi na kuwawezesha wakulima wetu kuwa na ahuweni ya maisha. Hatuhitaji kuimarisha bei ya mafuta maana hakuna hata tone la mafuta tunalozalisha sisi hapa nchini na hivyo bei ya mafuta ikiwa juu in athali zaidi maana kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kitahitaji kununua bidhaa hiyo toka nje. Hebu tuwe na furaha apale tunapoona na wakulima wetui wanapata fedha nyingi.

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top