Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

BREAKING NEWS: HAIKUWAHAI KUTEGEMEWA RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA MH MBOWE HADHARINI NIZ ZIDI YA ISHU HII NYETI MNO...

Rais John Magufuli  amewaambia wakazi wa mji wa Bomang’ombe katika Jimbo la Hai kuwa amewasamehe.

Alitoa kauli hiyo akiwa katika jimbo hilo la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe baada ya kuwaona baadhi ya wananchi wakiwa wameshika jani la “Sale” ambalo hutumiwa na wenyeji kuomba msamaha.

Jani hilo linaloheshimiwa sana na wachaga wa mkoa huo, ndilo ambalo mtu akimpelekea mtu aliyemkosea na kumuomba yaishe, anayeombwa kupitia jani hilo hana jinsi lazima akubali.

“Nawashukuru sana wote mliokuja na haya majani ya mti. Nafahamu maana yake na mimi nimewasamehe wote. Najua na ninyi mmenisamehe wote,”amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa.

Ingawa Rais Magufuli hakuweka bayana walichomkosea, lakini katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, Rais Magufuli alipata kura 29,341 wakati mpinzani wake wa karibu, Edward Lowassa akipata kura 49,125.

“Tushikamane kwa pamoja tujenge nchi yetu. Hakuna Mtanzania anayekula vyama, Mtanzania anataka maendeleo, anataka hospitali, barabara, anataka madawa, maji yapatikane umeme,”alisema Rais.

“Hii ndio maana niko hapa kwa ajili yenu, naomba mniamini na Serikali yangu tuko kwa ajili ya kuijenga Hai na Tanzania kwa ujumla. Aika mae, Aikambe (Asanteni sana),”alisisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kuwashukuru wakazi wa Jimbo hilo kwa kura alizosema ni nyingi na ambazo zilimuwezesha kuwa Rais na akawaahidi kuwa atawaletea maendeleo bila kujali vyama.

“Ninawashukuru sana nataka niwaahidi mimi nitawafanyia kazi Watanzania wote bila kujali vyama vyao, bila kujali makabila yao, bila kujali dini zao bila kujali hata sura zao,” alisema

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top