KAMISHNA Simon Siro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema msimamo wa Jeshi hilo kuhusu maandamano ya tarehe 1 Septemba yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), bado upo pale pale, anaandika Pendo Omary.
Zimebaki siku tano kabla ya kufanyika kwa maandamano na mikutano itakayoongozwa na viongozi wa Chadema ambao wameasisi operesheni ya Kupinga Udikteta hapa nchini (Ukuta).
“Rai yangu, wale wazalendo wa nchi hii, wasiopenda kupamabana na jeshi lao la polisi, ambalo li
nawalinda wao na mali zao naomba siku hiyo wasiingie barabarani.” Amesema Sirro na kuongeza.
“Tuwaachie wale watu wachache wenye nia ya kuleta fujo. Ambao wanataka kuonekana wanapambana na Jeshi la Polisi,nawakaribisha waingie barabarani na sheria itachukua mkondo wake.”
Aidha, Kamanda Sirro amesema jeshi hilo, limepata taarifa za kintelijensia kwamba, kuna watu wamepewa fedha Sh. 40,000 kwaajili ya kuandamana na kufanmya fujo siku hiyo.
Wakati polisi wakisema hivyo, Chadema kupitia mwanasheria wake mkuu, Tundu Lissu imesisitiza kuwa, itafanya maandamano ya amani kote nchini na waandamanaji hawatafanya vurugu zozote.
Wabunge wa Chama cha Wananchi – CUF nao, siku ya jana wametangaza kushiriki katika maandamano hayo maandamano hayo maarufu kama Ukuta.
Post a Comment