Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI NZITO: JUMA KASEJA ATOBO SIRI NZITO YA MANULA BOCCO NA KAPOMBE KUIHAMA AZAMA FC...

Golikipa wa zamani wa timu za Simba na Yanga ambaye kwa sasa anaichezea Kagera Sugar ya Bukoba Juma Kaseja alikuwa ni mmoja kati ya wageni waliyoalikwa katika kipindi cha Sports Bar cha Clouds TV kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusiana na soka la Tanzania.
Juma Kaseja kama moja ya wachezaji wenye uzoefu ambao wamewahi kucheza vilabu vya Simba na Yanga kwa mafanikio makubwa, aliulizwa swali kuhusiana na mtazamo wake kuhusu Shomari Kapombe, Aishi Manula na John Bocco kutoka Azam FC kwenda Simba anafikiri ni wakati sahihi?
“Sijui kuna vitu gani vimetokea ndani ya Azam na mimi nasikia tu kama mnavyosikia nyie kuna utaratibu umewekwa hakutakiwa kusajili mchezaji sijui zaidi ya Milioni 15 lakini tunasikia Mbaraka kachukua zaidi ya Milioni 15”>>> Kaseja
Juma Kaseja

“Mimi nadhani tu kuna vitu vimetokea kwenye mpira wa Tanzania vinataka kuwaondoa wale wachezaji ambao wanaonekana ni waandamizi kwenye timu na hivyo vitu mimi sidhani kama viko Azam tu hivyo vitu vipo kwenye mpira wa Tanzania kwa hiyo Azam wamevitoa kwenye hizi timu kubwa mbili nao wamevipeleka kwao”>>> Kaseja
“Kwanza heshima watu hawataki kuwapa heshima wachezaji, Bocco ni mchezaji mkubwa ndani ya Azam anatakiwa wampe heshima yake hata kama kulikuwa kuna tatizo la mambo ya hela sijui kiuchumi wangeweza kukaa nae chini na kuongea nae Bocco nae ni binadamu” >>> Kaseja
“Kama miaka yote kachukua hela nyingi anawezaje kukataa mwaka mmoja, bwana sasa hivi uchumi umeyumba lakini mwakani mambo yakikaa vizuri haina neno Bocco nae ni binadamu angeelewa”>>>Kaseja
“Unapokuja kumfanyia mchezaji mkubwa kama huyo ambaye kashajitolea sana kuisaidia timu kibinadamu hata yeye hawezi kuwa na furaha anaona kadharaurika na hivyo ni vitu ambavyo wamefanyiwa watu wengi sema kwa Azam Bocco ndio mchezaji wa kwanza lakini kwa hizi timu zingine kawaida” >>> Kaseja

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top