Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

MAONI YA ZITTO KABE BAADA YA KENYA KUZUIA GESI KUTOKA TANZANIA KUINGIA KWAO.

April 24 2017 iliripotiwa taarifa iliyodai kuwa Wizara ya Nishati ya Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia kutoka Tanzania kuingia nchini humo ndani ya siku 7, taarifa hiyo ilidai kuwa nia ya Serikali ya Kenya ni kuondoa vituo vya kujaza gesi ambavyo sio rasmi ambavyo vimeibuka katika maeneo mbalimbali ya nchi ambayo vinahatarisha usalama.
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ni mmoja wa viongozi waliotoa maoni yao kuhusu hatua hiyo ya Serikali ya Kenya ambapo amesema……..
Uamuzi huu wa Kenya ni kinyume na misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Tanzania na Kenya ni wanachama. Kwa mujibu wa Itifaki ya Soko la pamoja, bidhaa za nchi zetu zinaruhusiwa kusambaa ndani ya jumuiya bila vikwazo.
Gesi ya kupikia kuingia Kenya hutokea Tanzania Kwa sababu Tanzania ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo imewekeza mitambo ya kupokea Gesi na kuiweka kwenye mitungi. Bandari ya Dar Es salaam na mfumo mzuri zaidi wa kupokea gesi kuliko Bandari ya Mombasa na hivyo kuifanya gesi inayotoka Tanzania kuwa na gharama nafuu nchini Kenya kuliko gesi inayoagizwa kupitia bandari ya mombasa.
Uamuzi wa kuzuia Gesi kutoka Tanzania ni uamuzi wenye kulenga kuilinda bandari ya Mombasa Kwa kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kwa kutaka kuifanya Tanzania iendelee kuwa muuzaji wa malighafi kwenda Kenya badala ya bidhaa zilizokamili Kama gesi ya kupikia.
Uamuzi huu wa Serikali ya Kenya una lengo la kuathiri urari wa biashara kati ya Tanzania na Kenya ambapo Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa nyingi zaidi huko Kenya kuliko inazoagiza kutoka nchi hiyo.
Ninamsihi Waziri wa Biashara na Viwanda wa Tanzania afuatilie suala hili na kuzungumza na mwenzake wa Kenya ili waondoe vikwazo Hivi vya biashara ambavyo havina maana yeyote na vinazuia raia wa kenya kupata bidhaa nafuu kutoka Tanzania. Viwanda vingi vya Kenya hutegemea malighafi kutoka Tanzania, kuzuia gesi ya kupikia na kuendelea kuagiza malighafi za kuendesha viwanda vyao ni sera ya Kenya kuifanya Tanzania kuwa chanzo cha malighafi tu na sio chanzo cha bidhaa zilizoongezwa thamani.
Serikali ya Tanzania isikubali hili na ianze mazungumzo mara moja na Serikali ya Kenya ili Watanzania wanaouza gesi ya kupikia huko Kenya waendelee kuuza na kutumia Bandari ya Dar Es Salaam. Kama Serikali ya Kenya ikiendelea na msimamo wake basi Tanzania ichukue msimamo kama huo kwa bidhaa za Kenya Kama maziwa ambayo yamejaa kwenye soko letu

TAARIFA NZITO: HAKUNA ALIEAMINI HAYA HUKUMU YA BABU SEYA,PAPII MAPYA YAIBUKA LEO HII.


Tumaini jipya! Mtoto wa kiume wa mfungwa anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking ‘Babu Seya’, Mbangu Nguza ameibuka na kusema kuwa, mwaka 2017 ndiyo wa mwisho kwa baba yake na mdogo wake, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kuendelea kutumikia kifungo chao cha maisha jela.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Amani mwanzoni mwa wiki hii, Mbangu alisema kuwa, turufu ya mwisho ya hukumu ya ndugu hao ipo kwenye mikono ya Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCPHR) yenye makazi yake jijini Arusha ambayo kimsingi vikao vitatu vya awali vimeshakaa na kubaini kuwa, hukumu ya Babu Seya na Papii ilikuwa na kasoro.

“Unajua watu hawafahamu, kule ambako hukumu ya mzee na bwana mdogo (Papii), ilipelekwa kuna hatua. Kwanza kabisa, wale majaji wanatoka nchi mbalimbali, kwa hiyo siyo kwamba wanakwenda tu Arusha na kupitia hukumu, hapana.

“Kilichofanyika ni kwamba, kuna watu walikaa mara tatu kupitia hukumu ili wajiridhishe kama kuna makosa ambayo majaji wakikaa watayaona?“Kwa hiyo vile vikao vimeshakaa mara tatu zote na kubaini kuwa, kweli hukumu ya baba na bwana mdogo ilikuwa ina kasoro.

“Sasa ndiyo majaji wameitwa ili kupitia na kutoa hukumu yao ya haki. Hii kazi ingekuwa imeshafanyika muda mrefu ila sasa, kilichotokea ni kwamba, kuanzia Novemba mwaka jana kama sikosei, watu wa mahakamani walikuwa likizo ndefu mpaka kwenye Februari mwaka huu, ndiyo wamerudi.

“Kingine kimechelewesha ni mwaka jana kustaafu kwa rais wa ile mahakama, Jaji Augustino Ramadhani (kutoka Tanzania), kukawa na kitambo cha kusubiri kumpata rais mpya, tayari yupo (Sylvain Ore kutoka Cote d’Ivoire).

“Kwa hiyo bwana, baada ya sasa, wakati wowote ule, majaji watatua Arusha na kukaa kupitia, naamini, tena narudia kusema, naamini, baba na bwana mdogo wangu mwaka huu watakuwa huru.

“Hili suala la wao kuwa huru liko pia kiroho, hata kama mahakama hiyo isingekaa, bado wale ndugu wangetoka tu, lazima. Kwani Mungu ninayemtegemea mimi ameshaniambia watatoka,” alisema Mbangu ambaye kwa sasa ni Mwinjilisti wa Neno la Mungu.


TUMEFIKAJE HAPA?

Nguza na wanawe watatu walikamatwa Oktoba 12, mwaka 2003 na kufikishwa Kituo cha Polisi Magomeni, Dar, walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16, mwaka 2003 wakituhumiwa kubaka na kunajisi watoto 10.

Baada ya kusikilizwa kesi hiyo Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Addy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye kwenda jela maisha kwenye Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.

Januari 27, mwaka, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu.

Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo, Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao, Mabere Nyaucho Marando walikata rufaa ya pili ambayo ilitupiliwa mbali.

Mwaka 2010 waliomba tena rufaa ambayo marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu Februari, 2010. Mahakama iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha, ikawaachia huru watoto wake, Mbangu na Francis Nguza.

KAULI YA MWIJAGE KUHUSU KENYA KUPIGA MARUFUKU GESI YA TANZANIA YAWA MWIBA MCHUNGU KWA JPM.

Jana Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage amekiri kupokea taarifa za katazo lililotolewa na serikali ya Kenya juu ya uuzwaji wa gesi zinazotumika majumbani zinazotoka Tanzania na kusema wataalamu wa wizara wanazifanyia kazi taarifa hizo.

Waziri Mwijage ametoa taarifa hiyo wakati alipozungumza na mwandishi wahabari wa Azam Two mjini Dodoma baada ya kuzagaa kwa taarifa za serikali ya kenya kupiga marufuku ya gesi zamajumbani za Tanzania kuuzwa Kenya na kukiri kuwa Kenya wamekuwa na chokochoko kadhaa lakini watahakikisha wanakaa chini kutafuta suluhu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha viongozi wa juu wa nchi hizi mbili.
Download Video ya Gwajima Download Video ya Gwajima" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">

HABARI NZITO YA HIVI PUNDE MH ZITTO KABWE ACHANGANYIKIWA NA UNGA WABUNGE WENZIE WAFUNGA MAZITO MNO.

Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema bei ya unga wa ugali sasa ni juu kuliko hata bei ya mafuta ya magari jambo ambalo linafanya wananchi kuumia na gharama hizi za chakula.

Zitto Kabwe amesema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook na kusema bei hizi za chukula zipo juu sana na kufanya wananchi kuingia kwenye umasikini  

"Bei ya Unga wa Sembe 1kg TZS 2,300/= ( wastani ). Bei ya Mafuta ya Petroli 1lita TZS 2,060/= ( wastani). Kwa mara ya kwanza Ugali umekuwa ghali kuliko mafuta ya gari. Gharama hizi za maisha Kwa wananchi ni kubwa mno, hazistahmiliki na zinaingiza raia wengi kwenye umasikini. Serikali ipo kimya kana kwamba kila kitu kipo sawa" alisema Zitto Kabwe 

BREAKING NEWS: DIAMOND AFUNGUKA MAZITO JUU YA TUKIO HILI LA MWANADADA RAY C TENA..

Ikiwa ni siku chache baada ya Mwimbaji Ray C kuachia wimbo wake wa Unanimaliza, Leo Msanii wa BongoFleva, Diamond Platnumz kupitia account yake ya Instagram ameandika ujumbe huu…..
Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali….
Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya…. Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….
niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku🙏

HABARI NZITO:HALIMA MDEE AFUNGUKA MAZITO MNO JUU YA UHUSIANO WAKE NA SPIKA NDUGAI HAKUNA ALIEAMINI HILI.


Mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Halima Mdee jana amefunguka na kuomba radhi bungeni kufuatia kutoa lugha isiyokuwa na staha bungeni wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017. 
Halima Mdee wakati akiomba radhi hiyo anasema kuwa siku hiyo ya uchaguzi kulikuwa na matukio ambayo yalikuwa yakiendelea bungeni ambayo yalimpelekea kutoa lugha isiyokuwa sawa kitamaduni za bunge, ambayo ilimgusa Spika wa Bunge na Naibu waziri wa Wizara ya Afya, 
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala "Mhe. Mwenyekiti tarehe 4 mwezi wa 4 wakati wa uchaguzi wa EALA kuna matukio ambayo yalikuwa yanaendelea yakanipelekea kuzungumza lugha ambayo kitamaduni za Bunge si sawa na lugha husika ilimgusa Spika wa bunge na Mhe, Kigwangala kwa namna moja au nyingine kama mbunge mzoefu nilitumia jitihada binafsi kuzungumza na kuomba radhi wahusika katika 'individual capacity'lakini vilevile nikaona ni busara kwa sababu haya maneno niliyasema bungeni hivyo kuzungumza pia hapa na kumuomba radhi Mhe. Spika kwa hiyo niliomba huu muda kwa lengo la kumuomba radhi, kumwambia namuheshimu na kumwambia sitarudia" alisema Halima Mdee 

Mbali na hilo Halima Mdee aliendelea kuomba radhi kwa wabunge, watanzania pamoja na wananchi wa jimbo la Kawe lakini pia Halima Mdee alisisitiza kuwa michango yake ya bunge itaendelea kama kawaida yake lakini kwa kutumia lugha za staa

HAKUNA MATATA NAPE AZIDI KUITEKA CCM ATUMA UJUMBE HUU MZITO KWA RAIS MAGUFULI...

Leo April 26, 2017 Tanzania inaadhimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe zinazofanyika mjini Dodoma ambapo viongozi mbalimbali wamekuwa wakitoa pongezi kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kutimiza miaka hiyo.
Mmoja wa watu walioguswa na maadhimisho hayo ni Mbunge wa Mtama ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM na Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akitumia account yake ya Instagram na kuandika: CCM bado ni chama bora cha mfano kwa Afrika!!! Ni imara na kina historia ndefu, nzuri iliyotukuka sana!! Ndio waasisi wa Muungano wetu, TUUDUMISHE!!!!
#miaka53yamuunganowatanganyikanazanzibar.” – Nape Nnauye

KIMEWAKA MJINI DODOMA TUNDU LISSU AMTUPIA KOMBORA ZITO RAIS MAGUFULI AMPA MAKAVU NA KUMUITA JINA HILI TATA MNO.


Akiwasilisha bajeti kivuli ya wizara ya katiba na sheria.Mhe.Tundu lissu amesema ni aibu kubwa kama taifa kuwa na mhimili ambao haujakamilika kwa zaidi ya miezi 5

Lissu ametolea mfano mhimili wa serekali na bunge na kusema una viongozi wake.Rais kwa serekali na Spika kwa bunge wapo.

Amehoji iweje mahakama mpaka leo haina jaji mkuu?Amesema ni kumaanisha kuwa ma jaji wa mahakama kuu na rufaa na mawakili nchini wote hawana sifa ya kushika nafasi hiyo?Amesema vipi kuhusu majaji wa jumuiya ya madola?Si wapo kama nchini hamna mwenye sifa?

Amemaliza kwa kusema toka tumepata uhuru hamna rais aliicha mahakama bila jaji mkuu kwa kipindi kirefu kama Magufuli.

HATARI SANA EDO KUMWEMBE AWATUSI YANGA KIANA AFUNGUKA MAZITO JUU YA YANGA KUPITISHA BAKULI.

Jumatatu ya April 24 klabu ya Yanga ilizindua mpango wa kuomba mashabiki na wanachama kuichangia timu yao ili kuiwezesha kiuchumi, kila mmoja anafikiria wazo lake lakini moja kati ya watu ambao wamelipokea kwa utofauti ni mchambuzi mahiri wa habari za michezo wa Gazeti la MwanaSpoti Edo Kumwembe.
Haya ni mawazo ya Edo Kumwembe kupitia ukurasa wake wa facebook kuhusiana na suala la Yanga kuomba ichangiwe kwa njia ya simu na mashabiki wake.
“Yanga inaomba mchango kwa mashabiki wake? What a shame…mchango wa mashabiki wa Yanga ni kununua jezi original za timu na bidhaa kedekede zinazoambatana na jina lao. Mmewapelekea? Hapana. Mchango wa mashabiki wa Yanga ni kwenda kwa wingi viwanjani timu yao inapocheza ili wadhamini wajue ukubwa wa Yanga waipapatikie”
“Ni kweli mashabiki wanajitokeza na wadhamini wanaitamani Yanga, mdosi anabana ili aabudiwe, kamuulizeni jinsi Tiboroha alivyotimuliwa na mipango yake…kwa kuipenda Yanga tu kwa wingi wao tayari ni mchango tosha…walihitaji viongozi wa kutumia fursa hiyo Yanga iwe matawi ya juu sana”
“Leo viongozi wamerudi kwa mashabiki kutaka buku, nini maana ya kiongozi kama anashindwa kufikiria kuifanya Yanga iwe Tajiri? Yanga ya leo inaweza kuanzisha tournament ya siku tano tu ya pre season kwa kuziita Gor Mahia, Azam na Mamelodi ikauza TV rights kwa pesa kibao, ikapata wadhamini wa Tournament, ikapata viingilio vyote”

BREAKING NEWS: URAIS WA DR SHEIN WALETA KIZAAZAA KIZITO BUNGENI DODOMA.

Msemaji Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Ally Saleh jana alisusa kuendelea kusoma hotuba yake kwa madai kuwa hakuna uhuru wa kujieleza katika chombo hicho cha kutunga sheria.

Saleh alikatiza hotuba hiyo, baada ya kutakiwa kufuta kauli iliyohoji uhalali wa Dk. Ali Mohammed Shein kukalia kiti cha Rais wa Zanzibar.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali( AG), George Masaju alisema maneno yaliyotamkwa na Saleh hayapo katika uhalisia.

Masaju alisema Saleh anapaswa kurekebisha kauli yake kwa sababu Rais Dk. Shein alishinda uchaguzi mkuu uhalali.

Kufuatia ushauri wa AG, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Hassan Zungu alisema maneno yaliyomo katika hotuba ya upinzani yaliyosomwa na mbunge Saleh ni lazima ayatoe kwa sababu siyo maneno sahihi na hayapo katika uhalisia.

“Kwa hiyo maneno katika ukurasa wa tatu, kwenye namba tatu inatoka, kwa Dk. Shein inatoka kwa sababu alichaguliwa kihalali, ukurasa wanne wote," alisema Zungu.

Hata hivyo Mbunge Saleh aliamua kuondoka bila ya kuendelea kusoma hotuba hiyo na kusema kuwa uhuru katika bunge hauko kiasi cha kutosha.

Mbali na kuhoji uhalali wa Rais wa Zanzibar, wakati akisoma hotuba hiyo Saleh alidai wizara zinakiona cha moto, mawaziri wamebanwa mbavu na kwamba muungano siyo ajenda ya awamu ya serikali ya awamu ya tano kutokana na matendo ambayo yanatokea.

Alisema endapo hali hiyo itaendelea basi "kidagaa kitamuozea mtu mkononi na maiti atampakata yeye."

Mara baada ya kusoma sehemu hizo katika hotuba yake, ndipo Mwanasheria Mkuu Masaju aliposimama na kutoa taarifa na kusema kuwa Saleh anatumia maneno ambayo ni makali.

Masaju alisema Saleh anapaswa kurekebisha kauli kwa sababu hakuna wizara iliyokiona cha moto wala waziri aliyebanwa mbavu, pia Rais Dk. Shein alishinda uchaguzi mkuu kwa uhalali.

Kauli hiyo ya Masaju ilizua tafrani bungeni hali iliyosababisha baadhi ya wabunge upinzani kusimama na kuomba taarifa.

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alisema Mwanasheria Mkuu Masaju anapoteza muda kwa kuwa anazungumzia masuala ambayo hayapo kikanuni.

Naye Mbunge wa Iringa mjini (Chadema), Peter Msigwa alisema uhuru wa kambi ya upinzani upo kikatiba.

Alisedma bunge linaendeshwa kwa kanuni hivyo walio wachache wasikilizwe na walio wengi wanapswa kutoa maamuzi.

“Sasa Serikali hata sisi tuliowachache tunavyotoa maoni na mawazo tunazuiwa, hivi utamaduni wa bunge hili ni upi? AG badala ya kuisaidia Serikali ili inyooke amekuwa mtetezi, na bado anapotosha hapa," alisema Msigwa.

"Sisi ni upinzani na ndiyo kazi yetu, sasa kama kila kitu tunachoandika tunapingwa, mnataka tufanyeje? Hatujaja hapa kuwasikiliza nyie.
Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top