Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

‘Salaumu’ za UKUTA zaifikia Marekani

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
NCHI ya Marekani kupitia ubalozi wake nchini Tanzania, imepata taarifa za uwepo wa maandamano na mikutano ya kisiasa kote nchini mnamo Septemba Mosi mwaka huu na kuwatahadharisha raia wa taifa hilo, anaandika Charles William.
Operesheni ya kupinga kile kinachoitwa ‘udikteta unaoanza kumea’ hapa nchini, ilitangazwa mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu na Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema taifa, kwa niaba ya Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi kwa wingi mbili na kuibuka na azimio hilo.
Katika taarifa yake kwa raia wa Marekani waishio hapa nchini, ubalozi wa nchi hiyo umewataka raia wake kuepuka kujichanganya katika mikusanyiko ya maandamano ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
“Ingawa maandamano hayo yametangazwa na viongozi wa vyama vya upinzani kuwa yatakuwa ya amani lakini yanaweza kuibua vurugu kutokana na mvutano uliopo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza zaidi kuwa, “ingawa raia wa Marekani hapa nchini wamekuwa siyo walengwa katika maandamano yaliyopita lakini tunawatahadharisha kuepuka mikusanyiko ya watu na maeneo ambayo maandamano hayo yatafanyikia.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top