Kahama. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga katika makontena mbalimbali kwa lengo la kwenda kuzipima kwa wataalamu wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.
Taarifa iliyoletwa kwa vyombo vya habari na Ofisi ya Waziri Mkuu imeelza kuwa Waziri Mkuu alitaka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo una kiasi gani cha dhahabu, pia Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni sahihi.
“Hata hivyo tayari Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alishatoa tangazo la kuzuia usafirishaji wa michanga kwenda nje ya nchi,”alisema Waziri Mkuu katika taarifa hiyo
Waziri Mkuu alitembelea mgodi huo jana jioni (Jumatatu, Machi 27, 2017) na kuchukua sampuli za mchanga kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya kinachosafirishwa.
Sampuli hizo amezichukuwa kwenye makontena yaliyofungwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi
Download Video ya Gwajima
" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">
Post a Comment