Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HATARI SANA MZEE MWINYI AFUNGUKA MAZITO JUU YA TANZANIA YA AMGUFULI AMTUPIA DINGO HILI ZITO.

RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi amemuomba kiongozi wa dini ya Wahindu ya Swaminarayan Duniani, Mahant Swami Maharaji kuiombea Tanzania amani na umoja viweze kudumu na kusiwepo aina yoyote ya ubaguzi kwa sasa na hata vizazi vijavyo.

Mwinyi aliyasema hayo Dar es Salaam baada ya kualikwa katika hafla ya kumkaribisha kiongozi huyo hapa nchini na kukutana na waumini wa dini hiyo.

Pia ilikua ni maadhimisho ya miaka 40 tangu kujengwa misikiti miwili ya dini hiyo hapa nchini.

Alishukuru kwa kualikwa katika hafla hiyo ya kidini kwani sio jambo la kawaida kupokea ugeni wa kiongozi wa kidini nchini.

“Sina shaka kuwa sio nchi zote wenye kuwa na uwezo wa kumuona kiongozi mwenye nafasi kubwa kama hiyo katika nchi zote,” alisema na kuongeza kuwa kama Watanzania wengine amekuwa mwenye bahati.

Alimkaribisha kiongozi huyo nchini na kumtaka kuiombea sana Tanzania ili iendelee kudumisha amani na umoja na licha ya kutokuwepo kwa aina yoyote ya ubaguzi, aendelee kuomba ili hali hiyo isiwepo kamwe na wananchi waendelee kuishi kama ndugu.

Kwa upande wake, kiongozi huyo ambaye ni wa sita kwa nafasi hiyo, Maharaji alisema ataendelea kuiombea Tanzania na dunia nzima kwa ujumla ili wananchi wake waendelee kubarikiwa katika maisha yao pamoja na kukuza maendeleo yao.

Alisema mwanadamu siku zote hupenda raha lakini ni vyema wakafahamu kuwa hakuna raha kubwa kama kupata kutoka kwa Mungu kwa kuwa raha nyingine zote ni za muda, hazidumu.

“ Starehe ya mwanadamu ni ya muda mfupi na raha ya kuishi anayeitoa ni Mungu na ambayo haidumu, hivyo siku zote yapasa kuomba sana kwa Mungu kupata raha ya kudumu,” alisema na kusisitiza wajibu wa kila mwanadamu kuomba amani siku zote na kila wakati na kuishi kwa kanuni za Mungu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top