Anaandika mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mh Tundu Lissu!
Wakubwa habari za asubuhi.
I'm still licking my wounds, kama wasemavyo Waingereza.
Pamoja na kwamba vumbi la uchaguzi wa jana bado limetanda, naomba niseme yafuatayo juu ya uzoefu wa hizi siku chache zilizopita.
1) Kuna wanaodai tulikosea kutokuangalia gender balance ndio maana tumeshindwa.
Hapana.
Kosa letu sio kutokuzingatia jinsia. Kosa letu kubwa na lisilosameheka ni kuwa chama kikuu cha upinzani dhidi ya MaCCM. Na tumelifanya kosa hilo tangu mwaka 2010.
Wenzetu wa CUF nao walishawahi kufanya kosa hili kubwa miaka ya nyuma na mnakumbuka yaliyowapata. Na NCCR Mageuzi kabla ya CUF.
2) Kosa letu la pili ni kuwa chama kikuu cha upinzani lakini bila kuwa na nguvu ya kutosha bungeni kuzuia njama za MaCCM ndani na nje ya Bunge.
Ni hivi. Sisi wa UKAWA tupo 116, MaCCM yako 252 na bado wanajiongeza i.e. Salma Kikwete na wengineo watokao Magogoni. Wao wana 70%, sisi tuna 30% ukihesabu kila mtu aliyeko bungeni.
Kwa balance hii hata tukifanyaje tutaonewa tu. Na chochote tutakachopata itakuwa ni kwa fadhila yao.
Kwa sababu ya balance hii, hawahitaji hata kuheshimu sheria na kanuni za Bunge.
Kati ya Jumamosi na jana wamebadilisha sheria na kanuni za uchaguzi kwa namna ambayo inatisha.
In fact, hawakufuata chochote kilichoandikwa kwenye Kanuni za Uchaguzi wa Wabunge wa EALA. Badala yake, walibadilisha kanuni kadri mchezo ulivyokuwa unaendelea na kadri ya mahitaji ya maslahi yao.
Kanuni inavipa vyama vya siasa haki ya kuweka mgombea mmoja hadi watatu kwa kila nafasi inayogombaniwa. Ndivyo tulivyofanya. Machoni pao tulikosea sana.
Kwa practice ya Bunge letu, wagombea wasiokuwa na mpinzani hupita bila kupingwa. Na hii ndio sheria yetu ya uchaguzi hata nje ya Bunge. Jana imebadilishwa.
Wagombea wa CUF walikuwa wanne kwenye nafasi moja wakati kanuni zinasema maximum ni wagombea watatu kwa nafasi moja.
Watatu kati ya hao hawakuwa na fomu za uteuzi zilizosainiwa na Katibu Mkuu wa CUF kama ilivyotakiwa na kanuni. Bali, kwa kauli ya Katibu wa Bunge na Msimamizi wa Uchaguzi, majina yao yalitokea NEC.
NEC inahusikaje na uteuzi wa majina ndani ya vyama, mimi sijaelewa bado.
Kura zilipigwa kwa utaratibu usiokuwepo kwenye kanuni kabisa. Hakuna upigaji wa kura ya ndio au hapana kwenye uchaguzi wa EALA. Lakini wamepigia wagombea wetu au hapana.
Hakuna utaratibu wa wengine wanapigiwa kura ya ndiyo tu lakini wengine wanapigiwa ndio au hapana kwenye karatasi hiyo hiyo moja ya kura. Jana wagombea saba wamepigiwa kura za ndio tu, wawili wamepigiwa ndio au hapana.
Kanuni inasema usipochagua wagombea tisa basi kura yako imeharibika. Jana wamepigia kura wagombea saba tu na hakuna kura yoyote iliyoharibika.
Kanuni inaelekeza kura kuwa ya siri lakini jana usiku hakukuwa na kura yoyote ya siri.
Na mengine mengi.
Yote haya yanatokana na dominance ya MaCCM bungeni. Na juu ya yote haya, ongezea la Msimamizi wa Uchaguzi ambaye anajifanya ni refa wa mchezo huu lakini kiuhalisia ni kocha wa timu ya MaCCM.
Katika mazingira haya, je, watu hawa wataitisha uchaguzi mwingine ili kujaza nafasi mbili za CHADEMA zilizobaki???
Hili ni kwa wale wanaofikiria tukiongeza jina moja au mawili basi shida itakwisha na MaCCM yatatupatia nafasi zetu. Mimi sina jibu lake lakini hisia zangu zinaniambia hii imetoka.
Nitaendelea wakati mwingine.
Post a Comment