Ikiwa ni nje ya Zawadi zilizokuwa zimeandaliwa kwajili ya Washindi wa mashindano makubwa afrika ya kuhifadhi na kusoma Qur-an juzuu 30 Kati ya washiriki 17 kutoka nchi 15 Barani Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, Tanzania, Katika hotuba yake Mkuu wa mkoa wa jiji hilo Paul Makonda naye kwa upande wake alitamka kuongeza shilingi Milioni 5 kwenye zawadi za washindi watano waliopatikana.
Mohamed Abdullah Aden kutoka Somalia ndiye ameibuka mshindi wa mashindano makubwa Afrika ya kusoma na kuhifadhi Qur-an juzuu 30 amekabidhiwa hundi ya Shilingi Milioni 15 kutoka Amana Bank, halikadhalika amepewa cheti cha ushindi, Ipod na kuchagua kwenda nchi yeyote duniani, kijana huyo wa miaka 12 ametoa wito kwa vijana kujibidisha Katika kusoma Qur-an.
Mashindano hayo ya 18 yaliyo andaliwa na Taasisi ya Al-hikma Foundation yamehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa, Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeiry, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda, Skeikh Mkuu Dar es salaam Alhad Mussa Salum, Rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi Sambamba na ujumbe Maalumu kutoka nchini Saudiarabia.
Post a Comment