Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

Tony Blair ajitetea

Image copyright
Image captionTony Blair
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza , Tony Blair, amejitetea dhidi ya uamuzi alioufanya wa kuiingiza Uingereza katika vita ya Iraq mnamo mwaka 2003 kwa kushirikiana na mshirika wake Marekani baada ya ripoti ya tume ya uchunguzi kuhusu vita hivyo.
Bwana Blair amesisitiza kwamba hakuipotosha Uingereza kuingia katika vita hivyo, ingawa ameomba radhi kwa familia zilizifiwa na ndugu zao wakati wa vita hivyo.
Tonya Blair amesema anaamini kwamba ulikuwa ni uamuzi sahii wa kumuondoa kiondongozi wa zamani wa Iraq marehemu Saddam Hussein, na kwamba angeweza kuchukua uamuzi kama huo wakati huu.
"Wacha tuwe wazi kuhusu uamuzi. Inatokana na kilichotekea huko Mashariki ya kati. Na ninaamini kwamba Iraq ingepata utulivu na Mashariki ya Kati pia ingepata utulivu. Kuhusu tathimini yangu kwa yale yanayoendelea huko mashariki ya kati ni mapambano makubwa, kuondoa siasa za kidini na kuweka siasa zinazojumuisha watu wote,kuvumiliana, na kuvuliana dini za watu wengine. Na uamuzi huo ilikuwa na nia ya utawala unajenga uchumi sio uchumi wa ufisadi. Kwa sasa nafikiri hivyo ni vitu viwili, watu wanapambana eneo zima la Mashariki ya kati. Na Iraq chini ya Saddam haina nafasi." alisema
viongozi waandamizi katika maamuzi nchini Uingereza wameanza kurusha lawama kwa mshirika wao Marekani juu ya uamuzi uliochukuliwa mwaka 2003 dhidi ya vita vya Iraq kutokana na athari za uamuzi huo kuzidi kuonekana miaka kumi na nne baadaye.
Mapema wiki hii, Uingereza uchunguzi uliofanywa na John Chilcot umeegemea kuelekeza mashambulizi makubwa juu ya maandalizi,utekelezaji na matokeo ya vita vya Iraq.
Jenerali Tim Cross, mmoja kati ya viongozi waandamizi wa jeshi nchini Uingereza kushiriki katika mipango vita hivyo,Alisema Marekani inapambua jeshi la Iraq na chama cha Ba'ath zilivyoingia vitani bila kufuata ushauri.
Naye Jeremy Greenstock,balozi wa Uingereza Balozi katika Umoja wa Mataifa alinukuliwa akisema kwamba Marekani iliisukuma jeshi la Uingereza mapema mno, na kuongeza kusema kwamba wachunguzi wa umoja wa mataifa wanapaswa kutumia muda zaidi kuchunguza masuala ya kemikali na silaha za kibaiolojia zilizotumika katika vita vya Iraq .
Alistair Campbell,alikuwa mkuu wa kitengo cha mawasiliano wakati wa utawala wa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, amesema kwamba Wamarekani hawatekelezi makubaliano yaliyofikiwa kabla kama walivyotarajiwa .

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top