Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI NZITO: MAKONDA NAE MATATANI KAULI YAKE HII SASA YAMPONZA VIKALI BUNGE LAFIKIA MAAMUZI HAYA MAZITO ZIDI YAKE HIVI PUNDE.


Kubwa nyingine kutoka Bungeni Dodoma February 8 2017 ni maamuzi ya Wabunge kupiga kura za maazimio ya kuwaita kwenye kamata ya maadili ya Bunge Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti kwa madai ya kutoa lugha za kulidhalilisha Bunge.
Awali wabunge waliomba mwongozo kwa Mwenyekiti wa bunge Andrew Chenge akubali bunge kujadili kauli za Paul Makonda aliyetuhumiwa kwa kunukuliwa akizungumzia Wabunge >>> ‘Unajua zile ni mbwembwetu, wakati mwingine wale huwa wanachoka na kusinzia hivyo ni lazima wakati mwingine kuwe na watu akili zao zinasaidia kucheka’

Paul Makonda mbele ya Waandishi February 8 2017
Baadhi ya wabunge wakiwemo Abdallah UlegaEster BulayaMwita Waitara pamoja na Joseph Msukuma walisimama kuelezea Bunge namna walivyozipokea taarifa za Makonda huku wakiendelea kushinikiza bunge lizipokee hoja na kutaka kamati ya maadili itekeleze wajibu wake wa kumtaka kufika bungeni kwa ajili ya mahojiano.
Nje ya RC Makonda mwingine aliyedaiwa kutoa lugha za kudaiwa kudhalilisha bunge ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti ambae naye anadaiwa kurekodiwa sauti akikashifu utendaji kazi wa bunge , bunge liliafiki ajumuishwe kwenye tuhuma hizo na kuitwa kwenye kamati hiyo ya maadili.
Mwenyekiti wa bunge Andrew Chenge baada ya kuzisikiliza hoja zote za wabunge alitoa nafasi kwa Wabunge kupiga kura za Ndio au Hapana kuruhusu azimio la Watuhumiwa wote kuitwa mbele ya kamati ya maadili ya Bunge ambapo kura zote zilikuwa za Ndio.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top