Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI NZITO: KIMENUKA BUNGENI SPIKA JOBU NDUGAI AMTUMBUA RAIS MAGUFULI NA SERIKALI YAKE JUU YA SAKATA HILI NYETI NCHINI.

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameionya Serikali juu ya ucheleweshaji wa uwasilishaji wa mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo waTaifa, kiwango na ukomo wa bajeti.

Akizungumza bungeni jana muda mfupi kabla ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kuwasilisha mpango huo, Ndugai alisema kuwa kikanuni mpango huo unatakiwa kuwasilishwa Machi 11 ya kila mwaka.

“Kama ikiwa siku hiyo imeangukia siku isiyo ya kazi basi uwasilishaji huu hufanyika siku inayofuata. Mkija mwakani namna hii haitawezekana, hatutakuwa na mjadala,” alisema Ndugai.

Amewataka mawaziri, makatibu wakuu, maofisa wa Serikali na wabunge

kuhakikisha wanakuwapo mjini hapa kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa mpango huo kisekta na kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika kabla ya kuanza kwa mkutano wa Bunge Aprili 4 mwaka huu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top