Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

MBOWE AHIDI HILI JAMBO ENDAPO RAIS MAGUFULI ATASHINDA URAIS 2020.

magu
FREEMAN Aikaeli Mbowe, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho amesema atajiuzulu kufanya siasa iwapo Rais John Magufuli atashinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, anaandika Charles William.
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ametoa kauli hiyo mbele ya wanachama wa Chadema wilayani Muheza Tanga ambapo yupo katika ziara ya kukagua uhai wa chama.
“Huyu atakuwa rais wa kwanza kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano tu. Na kama Magufuli akishinda tena uchaguzi mwaka 2020 mimi nitajiuzulu siasa,” amesema Mbowe.
Amesisitiza kuwa chama chake tayari kimeanza kujiandaa na uchaguzi wa 2020 kwani kumalizika kwa uchaguzi mmoja ni maandalizi ya uchaguzi mwingine.
Mbowe yupo ziarani mkoani Tanga, akifungua matawi ya chama hicho na kukagua uhai wa chama. Ameambatana pia na Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha).
Mbowe ndiye mwanasiasa pekee ambaye bado anafanya siasa miongoni mwa waasisi wa mwanzo kabisa wa Chadema.
Wengi wamekufa na wengine ni wazee kiasi cha kutoweza kumudu mikimiki ya siasa za majukwaani.
Hii ni ahadi ya pili ya Mbowe kujiuzulu siasa.
Mara ya kwanza, mwaka 2014 aliahidi kujiuzulu siasa mwaka 2015 iwapo chama chake kingepata idadi ndogo ya kura za Urais na wabunge kuliko kilichopata mwaka 2010.
Hata hivyo Chadema kiliongeza Wabunge kutoka 49 mpaka 71 huku kura za urais zikipanda kutoka asilimia 26 kwa mwaka 2010 mpaka asilimia 40 kwa mwaka 2015.
source- mwanahalisionline

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top