Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta mapema leo ametupia picha kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter na huku akishukuru Mungu kwa kumwezesha kununua ndege ambayo itakuwa ikimsadia katika safari zake za masafa marefu ya ndani ya Bara la Afrika, Ulaya anakochezea soka na kwingineko Duniani.
Ndege hiyo ya kifahari ya kibinafsi ni miongoni mwa ndege zinazotumiwa na matajiri wakubwa Duniani hivyo kwa ununuzi huo, Mbwana Samatta anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kumiliki ndege hiyo.
Inadaiwa kuwa mchezaji huyo analipwa kiasi cha €35,600 kutokana na mkataba wake wa kuichezea timu ya Genk ambao utamalizika mwaka 2020.
Kwa sasa Samatta ameonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa kwenye timu ya KRC Genk ambayo pia inashiriki Michuano ya Europa League pamoja na ligi kuu nchini Ubelgiji.
Hata hivyo Mtandao huu wa MO Blog inawapongeza wasomaji wake wote kwa kuendelea kushirikiana nasi lakini pia tuwaondoe hofu tu, leo ni siku maalum ya Wajinga. (Foolish day) hivyo habari hii ni ya kuchangamsha pekee.
Post a Comment