Baada ya staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu kuvaa nguo zenye rangi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) alipotinga mahakamani hivi karibuni angali ni mwanachama damu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kisha baadhi ya wafuasi kudai anawasaliti, uongozi wa chama hicho umemtolea tamko.
ILIKOANZIA
Wema hivi karibuni akiwa ameongozana na mama yake, Miriam Sepetu na mashosti zake wengine, alitinga kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kwenye ile kesi yake ya ‘unga’ akiwa amevaa gauni refu la njano, juu akiwa amevaa ‘koti laini’ lenye rangi ya kijani na wekundu kwa mbali, hali iliyoibua mjadala kwa wafuasi wa Chadema waliokuwa mahakamani hapo.
“Huyu mbona leo katuvalia nguo hizi? Hizi si rangi za CCM kabisa? Mh! Kwa hili siyo sawa kabisa,” alisikika akisema mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa magwanda ya Chadema.
Mwingine akadakia: “Ni kweli rangi siyo ishu lakini kwa yeye ambaye juzijuzi alitangaza kuwa sasa ni Chadema damu, mavazi ya rangi hizi angeyachukia, sasa ona, utadhani ni kada wa CCM bwana.”
Kutokana na suala hilo kuibua maswali mengi kwa baadhi ya wanachama wa Chadema waliokuwa mahakamani hapo, Risasi Jumamosi liliwatafuta baadhi ya viongozi wa Chadema na kuwauliza kuhusiana na suala hilo ambapo kila mmoja alitoa tamko lake.
Meya wa Ubungo ambaye ndiye mlezi mkuu wa Wema Sepetu, Boniphace Jacob alisema; “Chadema siyo nguo, ni imani na itikadi kwani mahakamani lazima avae sare za Chadema? Hizo ni nguo tu kamanda, siyo ‘big deal’ sana.” Kwa upande wa msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene alieleza; “Hivi wale mashabiki au wanachama wa Simba wakivaa nguo za njano au kijani kwa sababu yoyote ile huwa ni ‘puppets’ (vibaraka) wa Yanga? Nadhani majibu hayo yamejitosheleza.”
Post a Comment