Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

RAPA KIPENZI CHA WATANZANIA ROMA NDIO BASI TENA HATIMAE AFUNGUKA SIRI NZITO YA KUTEKWA KWAKE HII LEO...


RAPA kipenzi cha Watanzania, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ amefunguka kuwa afya yake imeimarika na sasa yupo tayari kupanda jukwaani kukamua shoo kama kawaia yake.

ROMA ameyasema hayo jana wakati akitoa neno la shukrani kwa uongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Glopbal Publishers kwa kuendelea kumsapoti, kufanya naye kazi, kuboresha mahusiano yaliyo mema na kumfariji hasa katika kipindi kigumu alipopatwa matatizo ya kutekwa akiwa na wenzake watatu.

“Nimfika hapa kwa ajili ya kutoa neno la shukrani kwa jinsi ambavyo tmekuwa tukifanya kazi pamoja, pamoja na matatizo yaliyotukuta mimi na wenzangu lakini nyinyi Global Publishers mmeendelea kuwa na mimi katika kipindi chote hicho.

“Mtu akiona nimeweza kutembea kutoka nyumbani mpaka kufika hapa ofisini (Global PUblishers), basi ajue nipo fiti, na ninaendelea vizuri. kama nimeweza kushika maiki, nikazungumza basi hata Dar Live naweza kushika maiki (akimaanisha kufanya shoo).

“Niliona kipindi cha matatizo mlitupigania, magazeti ya Global Publishers yalifanya coverage nzuri na mlikuwa upande wetu. Kiukweli tulifarijika kuona watu wengi wakitutia moyo na kutupatia neno la faraja,” alisema Roma.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top