Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI YA HIVI PUNDE:..WATU WAKIMBIA MAKAZI BAADA YA HALI KUWA MBAYA, MACHAFUKO YAMEZIDI NA TAYARI MPAKA SASA WATU 70 WAMESHAPOTEZA MAISHA NA JESHI LAZIDIWA NGUVU

walinda amani wa CAR
Image captionWalinda amani wa CAR
Umoja wa Mataifa umekiri kwamba wanajeshi wake wa kulinda amani katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati walistahili kuimarisha utendakazi wake.
Hii ni baada ya ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International kusema wanajeshi hao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.
Mkuu wa kikosi hicho Parfait Onanga-Anyanga amesema kikosi hicho hakikutarajia kuzuka kwa ghasia katika mji mkuu Bangui hapo mwezi Septemba mwaka uliopita.
Raia wa CARImage copyrightAP
Image captionRaia wengi wamekimbia makaazi yao kutokana na vita CAR
Machafuko hayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 70. Wanajeshi hao waliweza kuzima ghasia hizo na kuweka mikakati mipya kuzima ghasia katika siku zijazo.
Bwana Onanga amesema wanajeshi wake walifanikiwa kusimamia ziara ya Papa hapo mwezi Novemba sawa na uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Decemba mwaka uliopita.
Jamuhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia kwenye vita vya kidini baada ya waasi waisilamu wa kundi la Seleka kupindua serikali mwaka wa 2013, na hivyo kuchochea machafuko ya kulipiza kisasi kutoka kwa wapiganaji Wakristo wa kundi la Anti-balaka.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top