Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

Waziri atengua uteuzi wa mkurugenzi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi),
Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mji wa Tunduma, Halima Mpita kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake.
Mpita anatuhumiwa kwa upotevu wa mapato ya Serikali yanayotokana na ushuru wa magari yanayosafiri nje ya nchi kupitia mpaka wa Tunduma pamoja na kuwaingiza watoto wake kazini kinyume cha sheria na kuwalipa posho.
Pia, Simbachawene aliagiza kusimamishwa kazi kwa wakurugenzi watatu wa halmashauri za Mbogwe, Misenyi, Nanyumbu na ofisa mmoja wa halmashauri ya Kilolo kwa tuhuma za kuwarubuni na kutoa rushwa kwa maofisa wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ili hati za halmashauri zao ziandikwe vizuri.
Baada ya kutengua uteuzi wa Mpita jana, amemteua aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa Mkoa wa Mbeya, Erick Mapunda kukaimu nafasi hiyo.
Alisema kwa nyakati tofauti mwaka jana, wakurugenzi hao walitoa fedha na kuwapa maofisa wa CAG, walipokuwa wakikagua halmashauri zao.
Alidai kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi, Kagera, Elizaberth Kitundu alimwagiza mweka hazina wake, Majaliwa Biakwaso kutoa Sh3 milioni kwa maofisa wa CAG ili wafiche kasoro walizozibaini.
Alidai katika Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara, Ally Kasenge akishirikiana na mweka hazina na mhasibu wake, walimpa Sh3.5 milioni ofisa wa ukaguzi wa CAG, F. Mwampashi ambaye alizipokea kwa niaba ya wenzake.
Pia, katika Halmashauri ya Mbogwe, Geita, alidai kuwa mkurugenzi Abdallah Mfaume na mweka hazina wake, Lukas Elias walitoa Sh16 milioni kwa maofisa watatu wa CAG ili kuficha udhaifu walioubaini katika ukaguzi.
Alisema katika mji wa Mbogwe, wakaguzi walibaini matumizi ya zaidi ya Sh200 milioni yaliyofanywa bila nyaraka muhimu za kuthibitisha matumizi hayo na kati ya fedha hizo, Sh144 milioni zililipwa kwa mkandarasi bila kazi iliyokusudiwa kufanywa. Pia, walibaini watumishi 82 waliohamishwa katika halmashauri bado walionekana katika orodha za mishahara.
Kuhusu Halmashauri ya Kilolo, alidai kuwa mtumishi wa idara ya fedha, Lackson Pina alimpatia zaidi ya Sh200,000 ofisa wa CAG Ili afumbie macho kasoro alizoziona kwenye mji huo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top