Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

Maoni ya RC Makonda baada ya Chadema kuahirisha UKUTA

Ni August 31, 2016 ambapo Chama cha Maendeleo CHADEMA kilitangaza kuahirisha mikutano, maandamano ya UKUTA kwa mwezi mmoja ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka.
Sasa hapa millardayo.com imempata Mkuu wa Mkoa wa Dar Salaam, Paul Makondakueleza maoni yake baada ya kuahirishwa kwa mikutano hiyo.
Maandamano hayajawahi kujenga shule, maandamano hayajawahi kuleta Elimu, maandamano hayajawahi kushusha vitu bei maduka bali maandamano ni Vurugu yaani kuondoka Amani na wale wanaodai demokrasia wanapaswa kwenda kutii tu kanuni zao za Bunge’
‘Kwahiyo kwenye mkoa wetu si tu tarehe 1 basi hakuna mtu kuzurura mahali popote pale, Ukuta ni kiwango cha mwisho cha mtu kufikiri sasa ndio maana wenzetu wameshindwa mwisho wa siku wanatafuta fursa kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka’
‘Mimi nafikiri naomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania afanye kazi na atekeleze aliyoyasema kipindi cha uchaguzi ili vijana afanye kazi katika viwanda mbalimbali tuachane na mambo ya UKUTA bali tuangalie vitu vya maendeleo’
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza RC Paul Makonda

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top