Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI NZITO YA HIVI PUNDE:RIPOTI NZITO YA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU KULIPASUA TAIFA VIPANDE VIPANDE HAKUNA ALIETEGEMEA MAJIBU YA SAKATA HILI NYETI...

Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya 4 barani Afrika kwa kuwa na vifo vya mama na mtoto huku ikiwa ya 6 duniani kwa vifo hivyo hivyo, suala ambalo wadau wa afya wanaishinikiza serikali kuwekeza katika huduma za dharura wakati wa kujifungua

Akiongea leo jijini Dar es salaam katika uwasilishwaji wa ripoti ya miradi ya afya katika mikoa ya Morogoro, Kigoma na Pwani Mkurugenzi wa shirika la Thamini Uhai Dkt. Nguke Mwakatundu amesema jitihada za makusudi za ujenzi wa huduma za dharura karibu na makazi ya watu hasa maeneo ya vijijini iongezwe ili kutatua changamoto hiyo.

“Nchi inayoongoza kwa vifo hivyo Afrika ni Nigeria, Democratic Republic of Congo, Ethiopia, Tanzania, na nje ya Bara la Afrika ni pamoja na India na Pakistan, kuna nchi nyingine zimeendelea lakini mila na desturi nayo nikikwazo kikubwa katika kuokoa maisha ya mama na mtoto” amesema

Dkt. Nguke amesema, wakati umefika kwa serikali kuhakikisha inatekeleza mipango mbalimbali iliyojiwekea katika kuhakikisha inapunguza vifo vya mama wakati wa kujifungua kutoka wanawake 332 kufikia idadi ya wastani ya wanawake 250 kama ilivyo ainisha katika mpango wa maendeleo wa Taifa ili kujiletea maendeleo.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Kinga ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia Wazee na Watoto Dr. Kaholeth Winani amesema, Asilimia 15 ya vifo vya mama na mtoto hutokana na matatizo yasiyo tabirika wakati wa uzazi hivyo ni jukumu la Jamii kutambua dalili za hatari na kuwawaisha kina mama kwenye vituo vya afya kwani asilimia 85 ya wajawazito hujifungua salama bila matatizo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top