Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI YA KUSIKITISHA: MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHUHUDIA MKASA HUU WA KUSIKITISHA MNO..


MAHAKAMA ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imemhukumu Francis Mganga (54) kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Leonard Nkola alisema amejiridhisha pasipo chembe ya shaka kuwa Mganga, mkazi wa Kijiji cha Isenegeja, alitenda kosa hilo.
Kutokana na hali hiyo, Alisema mahakama inamhukumu miaka 30 jela ili iwe fundisho kwake na watu wengine wenye tabia hiyo.
Awali, mwendesha mashtaka Frank Matiku, alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Mei 25, mwaka huu sasa saa mbili usiku.
Alidai kuwa mshtakiwa alimkamata kwa nguvu mwanafunzi wa darasa la pili anayesoma shule ya msingi Isenegeja na kumvutia kwenye nyumba yake na kumbaka huku akimtishia kuwa akipiga atamchoma kisu.
Mwendesha mashitaka alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha kifungu Na 130 na 131 cha kwanza cha Kanuni ya Adhabu Sura 16 mapitio ya mwaka 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo.
Baada yakusomewa mashtaka, Mganga alikana kutenda kosa hilo, ndipo upande wa mashtaka ulipopeleka mashahidi sita mahakamani na wote walimtambua mshitakiwa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top