Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HAKUNA ALIEAMNI HILI NDIO ZITO KUWAHI KUTOKEA KATIKA SIASA ZA TZ MAALIM SEIF, LIPUMBA WANATISHA KAMA UKOMA.

Licha ya mgogoro wa Chama cha Wananchi (CUF) kufikishwa mahakamani na Bodi ya Wadhamini ya chama hicho hivi karibuni kufungua shauri namba 23/2016 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake kwa madai kuwa wadaiwa hao wanashiriki kuihujumu CUF.

Bado mgogoro huo unaendelea ndani ya CUF kuanzia ngazi ya kata hadi taifa, ambapo viongozi waandamizi wa chama hicho ambao ni Katibu Mkuu Maalim Seif Sherif Hamad na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho aliyefutwa uanachama, Prof. Lipumba wameendelea kupeana tuhuma na kwamba kila mmoja anamtuhumu mwenzie kuwa na ajenda ya kukihujumu chama hicho ili kivunjike kitendo kilichosababisha wanachama na viongozi wa chama hicho kugawanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Maalim Seif amesema kuwa yeye sio sababu ya mgogoro uliopo sasa na wala hajahusika kumfukuza uanachama Lipumba bali CUF kupitia Baraza lake la Uongozi Taifa liliamua kumfuta uanachama kwa sababu ya kukiuka katiba ya chama hicho.

“Sina ugomvi na Lipumba, sijamfukuza, na niko radhi kufanya nae mdahalo ili aeleze siri ya kujiudhuru na kung’ang’ania uenyekiti wa CUF. Na hata tukipatanishwa haitasaidia kitu sababu, siwezi badilisha, chama ndicho kilichomfukuza kwa kura za wajumbe zaidi ya asilimia 70,” amesema.

Maalim amedai kuwa, Lipumba anatumiwa na baadhi ya watu kuuzima mgogoro wa uchaguzi uliotokea visiwani Zanzibar mwaka jana.

“Mgogoro huu wa CUF ni muendelezo wa hujuma zinazohusiana na kuzima harakati za kudai haki Zanzibar, ndio maana Lipumba analindwa na vyombo vya dola kuuendeleza mgogoro huu ili CUF ishindwe fuatilia mgogoro wa uchaguzi Zanzibar na kwamba wakubwa waonekane hawakukosea,” amesema.

Licha ya Maalim kumtuhumu Lipumba kutaka kuisambaratisha CUF, Jumamosi ya Novemba, 26 Prof. Lipumba katika mkutano wake wa ndani na baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji ya CUF wilaya ya Temeke, alidai kuwa Maalim na wafuasi wake wanapanga mikakati ya kukiuza chama na kwamba anahonga baadhi ya viongozi wa CUF kuanzia kata ili wamkatae kwa madai kuwa yeye ni kikwazo kwa Maalim kukiuza chama hicho.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top