Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HII YA LEO KALI: UBUNGO HAPATOSHI BAADA YA UKAWA KUCHUKUA UMEYA

Boniface Jacob, Meya wa Halmashauri ya UbungoVYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimetwaa Manispaa ya Ubungo leo, anaandika Pendo Omary.
Boniface Jacob (Chadema) ameshinda kiti cha Umeya wa manispaa hiyo jijini Dar es Salaam baada ya kupata kura 16 dhidi ya kura mbili za Yusuph Yenga, mgombea wa CCM.
Kwenye uchaguzi huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa manispaa hiyo uliopo Kibamba, Ramadhan Kwangaya, mgombea unaibu Meya kutoka CUF amepata kura 15 dhidi ya Kassim Lema wa CCM aliyepata kura tatu.
Meya Jacob baada ya ushindi amesema kuwa, atashirikiana na watendaji wote katika kuhakikisha analeta maendeleo kwenye manispaa hiyo mpya iliyogawanywa kutoka katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Katika Manispaa ya Kinondoni Jacob alikuwa Meya na sasa ni Meya wa Manispaa ya Ubungo baada ya uchaguzi wa leo.
“Nitaongoza kwa utatu mtakakatifu yaani watumishi, wanasiasa na wananchi. Nitasimamia mgawanyo wa Ubungo na Kinondoni na maswala yote yaliyopangwa katika bajeti inayoendelea, mikopo ya kina mama na vijana,” amesema.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top