Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

KIMENUKA MBAGALA MWENYEKITI AOMBA KUPIGWA RISASI YA KICHWA MBELE YA MAKONDA NI ZIDI KASHFA HI CHAFU.

Mwenyekiti soko la Mbande Mbagala katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Mokiwa Hassani ameomba kupigwa risasi mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda baada ya kutuhumiwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha katika upangishaji wa vizimba sokoni hapo. Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kufika sokoni hapo kwaajili ya kusikilizakero zinazowakabili wananchi ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake katika manispaa ya Temeke.

Unaweza ukadhani ni masihara lakini ndivyo hali halisi ilivyokuwa baada ya mkuu wa mkoa wa DSM kutoa nafasi kwa wakazi wa Mbande hususani wafanyabiashara wa soko hilo kutoa kero zao.

Kufuatia tuhuma hizo ikamlazimu mkuu wa mkoa kumsimamisha mwenyekiti wa soko hilo  Hassani ili kujibu tuhuma hizo ndipo alipotoa kauli hiyo na kufafanua kuwa bei hiyo ya shilingi laki nne kwa kizimba ni makubaliano kati yao na wananchi hao, pia fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kuendesha soko hilo, ambalo bado halijakabidhiwa kwa Halmashauri.

Kufuatia utetezi huo ikamlazimu Mkuu wa Mkoa kutumia busara ambapo ameuagiza mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kusimamia uundwaji wa uongozi wa soko hilo haraka mpaka kufikia mwezi Desemba kero zinazolikabili soko hilo ziwe zimetatuliwa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top