Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

LEMA NDIO BASI TENA RIPOTI NZITO YA KESI YAKE YAMTOA MACHOZI CHADEMA YATOA TAMKO LAO ZITO.

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameendelea kusota katika mahabusu ya Gereza la Kisongo mjini hapa akiingiza siku ya 22 leo baada ya jana kukwama katika azma yake ya kutaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kufanya marejeo ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha uliomnyima dhamana.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Moshi ndiye aliyetupilia ombi la Lema, hivyo kumfanya arejee mahabusu huku mawakili wake wakihaha kuhakikisha wanakata rufaa ili kuomba dhamana hiyo katika ngazi nyingine ya kisheria.

Aidha, Jaji Moshi ameridhia ombi la Lema kupitia kwa mawakili wake Sheck Mfinanga na Peter Kibatala la kukata rufaa mahakamani hapo ili kesi hiyo isikilizwe na hatimaye Lema kupata dhamana baada ya kupitiwa na jaji atakayepangiwa.

Akitoa uamuzi huo mahakamani hapo, Jaji Moshi alisema kimsingi hoja ya mawakili wa Lema ya kutaka mahakama hiyo kuitisha faili na kulipitia haina msingi wowote kisheria hivyo anaitupilia mbali hoja hiyo na kutoa rai kwa mawakili hao kukata rufaa Mahakama ya Rufaa ili dhamana ya Lema isikilizwe.

“Mahakama hii haiwezi kupitia faili la kesi hii ya Lema ya kupata dhamana hivyo siwezi kupitia faili hili, bali nashauri mkate rufaa ili iweze kusikilizwa,” alisema Jaji Moshi.

Awali Wakili wa Serikali, Paul Kadushi aliwasilisha pingamizi Mahakama Kuu la kuitaka wasisikilize maombi ya Lema ya kutaka mahakama hiyo iitishe faili la kesi namba 440/441 kwa madai yapo makosa ya kisheria yaliyofanywa awali na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa lengo la kumnyima dhamana mbunge huyo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top