Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HAKUNA ALIEAMINI KAULI NZITO YA MH LOWASSA YALITIKISA TENA TAIFA CHADEMA YAMUANGUKIA PROF LIPUMBA.

MGOGORO ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) unahusu vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anaandika Wolfram Mwalongo.
Kushindwa kutatuliwa kwa mgogoro huo si kuanguka pekee kwa CUF bali pia kuanguka kwa Ukawa. Ni kauli ya Edward Lowassa, aliyegombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuungwa mkono na Ukawa kwenye uchaguzi wa mwaka jana.
Kwenye ukurasa wake wa Facebook Lowassa amebainisha kwamba, CUF ni mshirika wa Ukawa na kuwa hata ushindi wa majimbo kwenye uchaguzi wa mwaka jana ni ushindi wa Ukawa.
Mara kadhaa Prof. Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa amekuwa akiwaaminisha wanachama wa chama hicho na wananchi kwamba Ukawa ni kirusi.
Kauli ya Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema inaibua hisia kwa wafuasi wa Ukawa kutoangalia mgogoro ndani ya CUF kama ni mgogoro wa chama hicho pekee.
Tayari Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema alitangaza msimamo wa chama hicho wa kutomtambua Prof. Lipumba kama mwenyekiti wa chama hicho.
“CUF ni wenzetu katika Ukawa, Shida zao ni shida zetu, vita vyao ni vita vyetu kushindwa kwao ni kushindwa kwetu, ushindi wao ni ushindi wetu,” ameandika Lowassa.
Ujio wa kauli hiyo unajenga taswira kwamba, mafanikio ya Ukawa kwa maana ya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi na NLD yanatokana na umoja huo na kwamba, kukubali kuuvunja ni kujimaliza.
Prof. Lipumba amekuwa akisema, Ukawa ni tatizo kwa CUF na kwamba, umoja huo unalenga kukimeza chama hicho cha tatu kwa wafuasi nchini huku akieleza kuchukizwa na ujio wa Lowassa Ukawa.
Kauli ya Lowassa inakwenda kinyume na kauli ya Prof. Lipumba ambaye anawaaminisha wananchi kwamba, Ukawa hususan Chadema ni kirusi kwenye umoja.
Pia kauli ya Lowassa inakuja ikiwa ni siku chache tangu Ukawa kueleza msimamo wake wakushirikiana na CUF katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Januari mwakani.
Pia Prof. Lipumba pamoja na timu yake wameeleza kusimamisha safu yake ya wagombea katika uchaguzi huo.
Prof. Lipumba alijiuzulu uenyekiti wa CUF Agosti mwaka jana kwa madai ya kukerwa na hatua ya Ukawa kumkaribisha Lowassa kupitia Chadema.
Pamoja na hoja ya Lowassa kujiunga Ukawa akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia Prof. Lipumba amekuwa akinadi kutokuwepo kwa usawa ndani ya Ukawa na kwamba hali hiyo inapunguza nguvu ya CUF.
Msimamo wa Prof. Lipumba umekipasua chama na kuwa kwenye makundi mawili makuu ikiwa ni moja linamuunga mkono yeye (Prof. Lipumba) na la pili likimuunga mkono Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa CUF.
Hatua ya kutaka kurejea kwenye nafasi hiyo baada ya kujiuzuli mwaka jana kwa kuandika barua, imekuwa msingi mkuu wa mgogoro ndani ya chama hicho. Hata hivyo Prof. Lipumba ameeleza malengo ya kutaka chama hicho kujitenga na Ukawa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top