Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI NZITO:LISSU NI SHIDAAHA AMNYOOSHA KAMANDA KUBWA WA POLISI MAHAKAMANI.

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani wamechuana mahakamani katika kesi ya uchochezi inayomkabili mbunge huyo na wahariri wa gazeti la Mawio.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba leo atatoa uamuzi wa kama Hamdani aeleze anachokifahamu juu ya Katiba ya Zanzibar na kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi  Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha anaweza kufuta matokeo ya uchaguzi.

 Hiyo ilikuwa ni baada ya Lissu kumtaka Hamdani, ambaye ni shahidi wa upande wa mashtaka, aeleze anachokifahamu kuhusu Katiba ya Zanzibar na kama Jecha anaweza kufuta matokeo ya uchaguzi.

Hakimu Simba alifikia uamuzi huo baada ya wakili wa Serikali, Paul Kadushi kupinga shahidi huyo kujibu swali hilo kwa sababu si mtaalamu wa sheria wala katiba hivyo hawezi kutoa tafsiri ya Katiba ya Zanzibar na kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza masuala ya kikatiba.

Lissu alimhoji Hamdani maelezo yake yaliyo polisi aliyaandika kama nani? Mahojiano yao yalikuwa kama ifuatavyo:

Hamdani: Niliandika maelezo yangu kama mlalamikaji na kwamba mikusanyiko hiyo haikuwa haramu, ilikuwa halali kisheria.

Lissu: Mweleze mheshimiwa kama mihemko kisheria inakatazwa ama la?

Hamdani: Haikatazwi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top