Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI NZITO: ASKOFU GWAJIMA AKAMTWA NA POLISI HIVI PUNDE SHUHUDIA TUKIO ZIMA NA MKASA WOTE HAPA.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (47) na wenzake watatu leo wataendelea kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali Joseph Maugo alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa kesi ilipangwa jana kwa ajili ya utetezi na wapo tayari. Wakili mwingine wa Serikali katika shauri hilo ni Shadrack Kimaro.

Washtakiwa wanatetewa na mawakili Peter Kibatala na Faraja Mangula ambao wote walikuwapo mahakamani jana lakini Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha anayeisikiliza kesi hiyo hakuwapo.

Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa utetezi.

Katika kesi hiyo, Gwajima anakabiliwa na shtaka la kushindwa kuhifadhi silaha na risasi anazomiliki kihalali katika usalama.

Washtakiwa wenzake George Mzava, Msaidizi wake, Yekonia Bihagaze (39) na Georgey Milulu wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa wakimiliki bastola aina ya Berretta na risasi 20 kinyume na sheria.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top