Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

KAULI YA RAIS MAGUFULI YALITIKISA TAIFA AFUNGUKA MAZITO MNO JUU YA MAUWAJI YA ASKARI POLISI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni tarehe 13 Aprili, 2017 katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi.

Mhe. Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP-Ernest Mangu, familia za askari wote waliouawa, Askari Polisi wote na Watanzania wote walioguswa na vifo hivyo.

“Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa, naungana na familia za marehemu wote, Jeshi la Polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu. “Namuomba Mwenyezi Mungu atupe moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amelaani tukio hilo na matukio yote ya kuwashambulia askari polisi ambao wanafanya kazi kubwa na muhimu ya kulinda raia na mali na ametaka Watanzania wote watoe ushirikiano katika kukomesha vitendo hivyo.

Mhe. Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.

1 comments:

HAKUNA MWANANCHI MWENYE AKILI, YAANI HATA ASKARI WETU NI WANANCHI PIA,.....MWENYE KUWEZA FURAHIA KITENDO HIKI AMA CHOCHOTE CHA UTEKAJI NYARA AU UPOTEAJI WA RAIA NA MBAYA ZAIDI KUUA RAIA KWA SABABU YOYOTE ILE!!....TUNAOMBA MAJESHI YETU, USALAMA WA TAIFA NA WANANCHI KWA UJUMLA TUJIRUDI TULIPENDE TAIFA LETU TUKUFU NA WATU WAKE TUPEANE SABABU YA KILA MOJA KUHESHIMIKA NA KUKUBALIKA KATIKA UTU NA HAKI ZAKE KIRAIA KIKATIBA NA KISHERIA ..... TUMPE KILA MOJA WETU SABABU YA KUONA ANA NAFASI SAWA NA KILA MWINGINE KAMA RAIA KIUTENDAJI NA KIUONGOZI MRADI HAVUNJI SHERIA ZA NCHI NA ANA UWEZO KIFIKRA NA KIDEMOKRASIA KUWA HIVYO BILA ATAHRI KWA JAMII KIMAENDELEO KIUCHUMI KISIASA NA KIUSALAMA!!
WATANZANIA TUNAHITAJI KUOMBA NEEMA KWA MUNGU ZAIDI YA AKILI ZETU BINAFSI JUU YA YOTE YALIYOTOKEA HUMU NCHINI, HILI LA MAUAJI YA POLISI WETU WAPENDWA, LILE YA KUPOTEA BEN SAA NANE NA YALE YA UTEKWAJI RAIA BILA MLISHONYUMA WA SABABU ZA MSINGI KWA MATUKIO HAYO NA MENGINE MENGI. KWA HAYA NITAOMBA MUNGU AYASHUGHULIKIE YOTE KWA UJUMLA WAKE NA SIO MOJA TOFAUTI NA LINGINE HADI HAKI AMANI UPENDO NA UMOJA WA KITAIFA KISIASA KIDINI NA KIJAMII VIKAHESHIMIKA CHINI YA ADABU ZA KUTII KATIBA NA UTAWALA WA SHERIA NCHINI TANZANIA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WEKA ROHO ZA ASKARI WETU SALAMA KWA MAPENZI YAKO MWNYEWE, MUNGU TUTUNZIE WALIOPOTEA NA HATUJUI WAPO WAPI. BEN SAA NANE SALAMA KWA NGUVU ZAKO ZOTE.....AMEN!

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top