Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

KUTOKA IKULU: KWELI HUYU MZEE HATARI HII NDIO KAULI YENYE UJUMBE MZITO KWA AJALI YA WANAFUNZI HAPO JANA..

Rais John Magufuli ametoa salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki kwa vifo vya wanafunzi, walimu na dereva vilivyotokea leo saa 3.00 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Rais Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo hivyo  vya wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 na dereva wa gari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha.

Wanafunzi na walimu hao walikuwa wakitoka shuleni kwao kwenda shule ya msingi iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofika katika eneo la Rhotia Marera basi walilopanda liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni ambako limesababisha vifo hivyo na majeruhi watatu.

Kufuatia ajali hiyo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Gambo na kueleza kuwa ajali hiyo imezima ndoto za watoto waliokuwa wakijiandaa kulitumikia Taifa na imesababisha uchungu, huzuni na masikitiko makubwa kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla.

“Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo naomba unifikishie pole nyingi kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wote wa wanafunzi, walimu na dereva waliopoteza maisha, hiki ni kipindi kigumu kwetu sote, na uwaambie naungana nao katika majonzi na maombi.

“Muhimu kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema, majeruhi wapone haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira, ustahimilivu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu,” amesema Rais Magufuli.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top