Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

MAAMUZI MAZITO YA JUMA KASEJA BAADA YA KUAMUA KUSTAAFU SOKA AFUNGUKA MAZITO MNO LEO HII..


Mlinda mlango mkongwe hapa nchini ambaye sasa anachezea Kagera Sugar Juma Kaseja amepanga kuwa mtangazaji wa radio au televisheni baada ya kustaafu kucheza soka.

Juma Kaseja amesema hayo alipokuwa akihojiwa na kusema atakapostaafu kucheza soka ataingia rasmi katika kiwanda cha utangazaji, ambapo awali ataanza kwa kutumia kipaji chake lakini kadri siku zinavyozidi kwenda itabidi aingie shule ili kuwa mtangaji mzuri zaidi na bora.

"Kila kitu kinahitaji elimu, ila mimi kwanza nitaanza hivi hivi nilivyo halafu kadri nitakavyozidi kwenda nitakuwa najiendeleza na shule ili niwe mtangazaji mzuri" alisema Juma Kaseja 

Mbali na hilo Juma Kaseja amesisitiza wachezaji wadogo wanaokuja kwenye soka wanapaswa kuwa wavumilivu, wasikivu kwa walimu wao na kuwa na nidhamu kama wanapokuwa kwa wazazi wao.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top