Handeni. Siku moja baada ya majambazi kumuua mlinzi katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (Sekomu), Tanga, majambazi ambao idadi yao haijafahamika, wamefunga Barabara ya Segera – Chalinze katika Kijiji cha Kwachuma wilayani Handeni kwa zaidi ya saa mbili na kupora fedha na simu za abiria waliokuwa kwenye magari usiku wa kuamkia jana.
Katika tukio hilo, watu watano walijeruhiwa kwa mapanga na kupelekwa Hospitali ya Magunga Korogwe.
Juzi, majambazi yalivamia Sekomu na kulipua moja ya mabweni ya chuo hicho, kisha kumuua Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Tele Security, Yohana Shemzigwa na kumjeruhi mlinzi mwenzake, Abuu Rajab.
Akizungumzia tukio la usiku wa kuamkia jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema majambazi hao walifunga barabara saa tano usiku kwa kutumia magogo kisha kuanza kuwapora mali watu waliokuwa wakipita kwa magari eneo hilo.
1 comments:
Tatzo hamuwek chanzo cha habar na hii ndio source ya blog kuishwa vistor c0unter
ReplyPost a Comment