Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

BREAKING NEWS: HUYU NDIE MBUNGE MACHACHARI MWANAMKE WA UPINZANI AJITANGAZA LEO HII KUISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI.

Image result for bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania

Novemba 27 hadi 29 Tanzania ilipata ugeni wa rais wa Zambia Edgar Lungu aliyetembelea nchi kwa ziara ya kikazi. Rais Lungu anatoka nchi ambayo inashujaa anayefahamika kwa jina la Princess Kasune mmoja ya wanaharakati maarufu wa ugonjwa wa ukimwi nchini Zambia na alichaguliwa kama mbunge wa upinzani mwezi Agosti.

Kwasasa Kasume ana umri wa miaka 40 aligunduliwa kuwa na virusi vya HIV mwaka 1997. Moja ya kitu ambacho mila na tamaduni za eneo analotoka zinapinga ni mtu kuweka hadharani hali yake ya maambukizi ya HIV. Kasume hakujali tamaduni zile mnamo mwaka 1998 akiwa na miaka 18 alitangaza hadharani hali yake pamoja na mmewe kupinga uamzi huo.

Kasume aliieleza BBC kuwa baada ya kugundua kuwa ana maambukizi ya HIV basi alitambua moja kwa moja kuwa ana jukumu la kuelimisha umma juu ya namna ambavyo unaweza kuambukizwa,kujikinga pamoja na kuondoa unyanyapaa kwa waathirika. Mbunge huyo wa upinzani aliwapoteza wazazi wake wote kwa ugonjwa wa Ukimwi akiwa na umri wa miaka 14 na kisha akaolewa akiwa na umri wa miaka 18.

KASUME

Moja ya hatua ngumu aliyopitia mwanaharakati katika kuhakikisha kizazi chote kiakuwa salama dhidi ya HIV ni kufukuzwa na kanisa lake baada ya kuweka wazi hali yake akidaiwa kwenda kinyume na matakwa ya mmewe kuhusu kuweka siri juu ya hali yake ya kuishi na virusi vya ukimwi.

Katika kuhakikisha anaieleza dunia ukweli kuhusu HIV, Kasume amekukutana na viongozi mbalimbali wakiwemo marais wa zamani wa Marekani,Bill Clinton na George W Bush pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top