Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

BREAKING NEWS: MSIBA MZITO TANZANIA YAPATA MSIBA MZITO MNO MZEE PINDA AFARIKI DUNIA.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa jana aliongoza mamia ya waombolezaji kumuaga baba mzazi wa Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, Mzee Xavery Mizengo Pinda (90) huku Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akimuelezea mzee huyo kwamba alikuwa mtu mkarimu na Mcha Mungu.

Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifanyika nyumbani kwa Waziri Mkuu mstaafu Pinda kwenye Kijiji cha Zuzu mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, viongozi wa chama na serikali, viongozi wa dini na wananchi.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema serikali itaratibu shughuli zote na itawakilishwa kwenye maziko na Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Mlele, Isaack Kamwelwe.

“Niliwahi kufika hospitalini kumuangalia kwa kweli hali yake haikuwa nzuri, tumuombee apumzike kwa amani,” alieleza Kikwete na kuongeza kuwa wakati akiwa Rais alifanya ziara Mkoa wa Katavi na alipita Kijiji cha Kibaoni kumsalimia mzee huyo. “Alikuwa ni mtu mwema na mwenye upendo mkubwa, alikuwa akitambua ugumu wa kazi za uongozi wa taifa alituombea. Alisema uongozi ni kuvumilia na kupokezana kijiti,” aliongeza Rais mstaafu Kikwete akimkariri Mzee Pinda.

Alisema Pinda alimpa taarifa za kifo cha baba yake na kufika ili kumuaga marehemu. Waziri Mkuu mstaafu Pinda akizungumza alisema kuondokewa na baba si jambo rahisi, lakini anamshukuru Mungu kwa kila jambo.

“Siku za mwisho za uhai wake zilikuwa nzuri, lakini mimi nilijua haiwezekani tena.” Akiongoza ibada nyumbani hapo, Padri Chesco Msaga wa Kanisa Katoliki alisema kila mwanadamu anatakiwa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu, wakati Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa alisema Mzee Pinda alitumia uhai wake vizuri na aliyoyaacha yaendelee kuokoa walio wengi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top