Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HILI NDIO TUKIO ZITO ALILOFANYA PM MAJALIWA NI BAADA YA MIAKA 20 KUPITA LEO HII WAZIRI MKUU AFANYA MAAJABU MAZITO.



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 17 kati ya vijiji viwili vya Ortukai na Esilalei na Taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust (TLCT) baada ya kukabidhi hati ya shamba la Manyara Ranch kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Stephen Ulaya.
Hati hiyo imetolewa jana jioni (Jumapili, Desemba 4, 2016) na Waziri Mkuu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mto wa Mbu kwenye viwanja vya Barafu baada ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kwenda kwa wananchi wa vijiji hivyo vilivyopo kwenye Kata ya Elesilalei Wilayani Monduli Mkoani Arusha.
Hatua hiyo imekuja baada ya kilio cha muda mrefu cha wananchi hao kudai kuwa Rais wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa aliagiza shamba hilo ligaiwe kwa wananchi hao lakini jambo hilo halikufanyika na badala yake watu wachache walijimilikisha shamba hilo kinyemela chini ya wenyekiti wa bodi ya TLCT.
Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kurudisha umiliki wa shamba hilo kwa wananchi wa vijiji hivyo viwili baada ya Baraza la Madiwani na Uongoziwa Wilaya hiyo ya Monduli kuridhia kwa pamoja umiliki huo kurudi kwa wananchi kama ilivyoamriwa hapo awali.
"Shamba hili lenye ukubwa wa ekari 44,930 sasa si mali tena ya Taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust (TLCT) iliyokuwa inafadhiliwa na Shirika la African Wildlife Foundation (AWF) sasa ni mali ya wananchi na halmashauri ya wilaya ya Monduli ndio itapanga matumizi bora ya ardhi ya shamba hili mliloteseka nalo kwa muda mrefu ," alisema

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top