Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

BUNGE LAZIDI KUTIKISA NCHI HIKI NDICHO KILICHOTOKEA BAADA YA SPIKA KUTAJA JINA LA SOPHIA SIMBA.




Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ametangaza rasmi kuwa kiti kimoja cha ubunge  Viti Maalum Wanawake kwa tiketi ya CCM kiko wazi kufuatia Mbunge wa nafasi hiyo Sophia Simba kufukuzwa uanachama wa chama hicho.

Kutokana na taarifa hiyo ambayo Spika wa Bunge amemjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, nafasi hiyo inapaswa kujazwa ambapo kwa mujibu wa Ibara ya 67 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ili mtu ateuliwe au achaguliwe katika nafasi ya Ubunge ni lazima awe mwanachama aliyependekezwa na Chama chake husika cha Siasa.
Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imesema

"Kwa kuwa Ndg. SOPHIA MNYAMBI SIMBA amefukuzwa uanachama wa Chama kilichomdhamini, Ibara ya 67 (2) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaelekeza kuwa Mbunge huyo amepoteza sifa za kuteuliwa au kugombea Ubunge".

Taarifa hiyo imesema kuwa pia kuwa kutokana na kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge wa Viti Maalum, taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top