Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

BREAKING NEWS: HATIMAE MH KINANA ATOKA MAFICHONI ATOA KAULI HII NZITO KWA WANACCM WOTE..

Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa Katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana alikuwa akiugulia afya yake pindi yupo kazini hivyo alichukua muda wa kutosha kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu.

Polepole amezungumza na AZAM NEWS ambapo alisema tangu Mzee Kinana akiwa hata kwenye mkutano mkuu wa CCM Dodoma hakuwa sawa kiafya.

“Tangu akiwa kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM Dodoma hakuwa sawa kiafya, alikuwa anafanya yote haya akiugulia afya yake kwahiyo ikakubalika achukue muda wakutosha wa kuitizama afya yake nje ya nchi na anapo rejea mgonjwa akitoka hospitali huwa hakimbii kazini, shambani moja kwa moja inashauriwa kitaalam atumie muda wa kupumzika ili kuimarisha afya yake na nimezungumza nae anaendelea vizuri yuko madhubuti kabisa kuliko jana,” alisema Polepole.

Katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana hajaonekana hadharani kwa muda tangu Rais Magufuli aliposema kuwa yuko India.

1 comments:

Kinana likizo ya Kuumwa???..."baada ya kufanya shughuli nyingi za chama na serikali.Imezoeleka kiongozi yeyote anapougua viongozi wenzake kwenda kumjulia hali hospitalini anakopatiwa matibabu au nyumbani kwake, lakini kwa Kinana imekuwa ni tofauti.Hadi sasa hakuna picha yoyote inayomwonyesha kiongozi au mtu yeyote amefika nyumbani kwa Kinana kwa ajili ya kumjulia hali, jambo ambalo limezidi kuzua maswali."...Kweli??...Mbona hili hatulisikii la kutembelewa na kujuliana hali??...Au limesikia wapi?

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top